Saturday, July 14, 2012

YANGA HOI KWA BAO 2-0

Kwenye lango la Atletico

MABAO mawili ya yaliyo fungwa na Olivier Ndikumana katika dakika ya 81 na
90+3, yameipa Atletico FC ushindi wa 2-0 dhidi ya mabingwa watetezi,
Yanga katika mechi ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga leo ilizidiwa katika kila idara-
angalau baada ya kufungwa bao la kwanza walijaribu kushambulia kwa mipira ya
pembeni, lakini walipopigwa la pili katika dakika ya tatu ya muda wa nyongeza
baada ya kukamilika kwa dakika 90 za mchezo huo ‘walitepeta kabisa’.
Katika mechi ya kwanza ya kundi hilo, APR ya Rwanda
iliitandika 7-0 Waw Salam ya Sudan Kusini.

Baada ya mechi hiyo, kocha wa Yanga, Tom Saintfiet alisema kwamba Atletico ni timu nzuri na walicheza vizuri, lakini timu yake haikuwa vizuri leo. Aidha, alisema alipokuja Yanga aliambiwa timu hiyo inacheza mpira wa kukimbiza, ambao yeye hakuutaka.

"Nataka wacheze soka ya utulivu, lakini leo mambo hayakuwa mazuri, taratibu timu itaendelea kuimarika na bado nina matumaini ya kufanya vizuri,"alisema.

Lakini kocha wa Atletico, Kaze Cedric aliiponda safu ya ulinzi ya Yanga, kwamba ilikuwa butu. "Niliiogopa Yanga, nilijua ina wachezaji wazuri, tulijua tutapata upinzani mkubwa, lakini nashukuru tumeshinda. Tulijua Yanga wana kasi, tukaanza kwa kuwatuliza,"alisema Kaze.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU