Saturday, July 14, 2012

REDD'S MISS SINZA 2012 NI BRIGITA ALFRED

 Redd's Miss Sinza 2012, Brigita Alfred (katikati) akipunga mkono kwa furaha wakati akiwa na washindi wenzake, mshindi wa pili Judith Sangu (kushoto) na watatu Esther Mussa, baada ya kutangazwa washindi katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mawela Social, Sinza Jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Kampuni ya SPM-Sufiani Photo Magic na Mtandao wa Sufianimafoto.blogspot,com, Nasma Sufiani, akimvisha taji na kumkabidhi zawadi Maria John, baada ya kuibuka kidedea katika shindano la kumsaka Sufianimafoto Miss Talent, lililofanyika ndano ya shindano hilo la Miss Sinza katika Ukumbi wa Mawela Social, Sinza jijini Dar es Salaam.
 Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya Tano Bora, wakipozi kwa picha, kutoka (kulia) ni Brigita Alfred, Judith Sangu, Nahma Said, Ester Mussa na Mariam Miraji, baada ya kutangazwa kutinga hatua hiyo.
 Sufianimafoto Miss Talent, Maria John, akiwa na furaha baada ya kuvishwa taji hilo na kukabidhiwa zawadi yake.
 Madj wa Sufianimafo, wakiwa katika mitambo ya Sufianimafoto, iliyokuwa ikitumika katika shindano hilo, wakiendesha shughuli nzima ukumbini hapo.
 Waimbaji wa Twanga Pepeta, wakishambulia jukwaa.
 Wanenguani na waimbaji wa Twanga, wakishambulia jukwaa.
 Mwalimu wa waremabo hao, Mwajabu Juma, akipita jukwaani kusalimia wadau wa urembo.
 Warembo wakicheza shoo ya pamoja ya ufunguzi.
 Miss Sinza 2011, (kushoto) akipozi na wenzake ukumbini hapo.
 Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya wanakamati wakishuhudia shindano hilo.
 Msanii wa Vichekesho, ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Uongo Kweli, akishambulia jukwaa, wakati wa onyesho hilo na kuwapagawisha vilivyo, mashabiki wa fani ya urembo waliokuwapo ukumbini hapo.
 Sehemu ya watu waliojitokeza kushuhudia shindano hilo.
 Sehemu ya watu waliojitokeza kushuhudia shindano hilo.Picha zote na Sufiani Mafoto Blog.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU