Saturday, July 21, 2012

SIMBA NA AS VITA ZATOKA SULUHU 1-1

 
 Kiungo mshambuliaji wa Simba, Amri Kiemba (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa As Vita, Mfongang Alfred, wakati wa mchezo huo.


Wakati wa mchezo wa kundi A, wa Kombe la Kagame uliomaliika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1. As Vita ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kwa njia ya mkwaju wa penati katika dakika ya 35 ambapo goli hilo lilifungwa na Etekiama Taddy. Simba nao waliweza kusawazisha bao hilo katika dakika ya 66 kupitia mshambuliaji wake Haruna Moshi 'Boban'.
 Juma Nyoso wa Simba (kushoto) akimchezea rafu mcheaji wa As Vita, Etekiama Taddy, wakati wa mchezo huo leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa.
 Mshambuliaji wa As Vita, Magola Mapanda (kulia) akiwania mpira na beki wa Simba, Juma Nyoso, wakati wa mchezo huo.
Kipa wa Simba, Juma Kaseja, akichungulia mpira uliopigwa kwa mkwaju wa penati na Etekiama Taddy na kuandika bao katika dakika ya 35 ya kipindi cha kwanza. Simba wamekosa penati katika dakika za majeruhi baada ya Sunzu kupiga fyongo na kuokolewa na kipa wa AS Vita na kufanya matokeo kuwa 1-1.


YANGA KUCHEZA NA MAFUNZO, SIMBA NA AZAM
WAKATI huo huo tayari Shirikisho la mpira wa miguu Tff, limekwishatoa maamuzi kwa kurusha shilingi na kumpata mshindi wa kwanza na wa pili katika kundi B, ambapo Yanga sasa itacheza na Mafunzo siku ya jumatatu na Azam kuchea na Simba na As Vita watacheza na Atletico. Picha na sufian Mafoto

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU