Tuesday, July 24, 2012

SIMBA YATUPWA NJE YA MASHINDANO YA KOMBE LA KAGAME


Mshambuliaji wa Simba, Uhuru Suleiman (kulia) akichuana na beki wa Azam, Said Moradi wakati wa mchezo huo leo.
 Kipa wa Azam,Deogratius Munisi akiondoa hatari iliyokuwa ikielekea langoni kwake
Mshambuliaji wa Azam,Kipre Tchetche akiwazungusha Mabeki wa Simba katika mchezo wao uliopigwa jioni hii Uwanja wa Taifa Jijini Dar


Katika mchezo huo Azam imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Simba, ambapo mabao yote yamewekwa kimiani na John Boko. 

Kwa matokeo hayo sasa Simba itakuwa imeondolewa katika mashindano hayo, ambapo Azam sasa itacheza na timu ya AS Vita siku ya Alhamis katika hatua ya Nusu Fainali ya michuano hiyo na Yanga itakutana tena kwa mara ya pili na APR ya Rwanda katika hatua hiyo ya Nusu Fainali baada ya timu hizo kukutana katika hatua ya robo fainali na APR ikikubali kichapo cha  mabao 2-0. 

1 maoni:

Anonymous said...

haya ndiyo matatizo ya kuzoea kuhonga mechi za ligi za bongo na makombe ya mbuzi.viongozi wa simba mkubali kubeba lawama ,hatutaki kuwasikia mkihusisha tff na kufungwa kwenu.nyie mnapenda sifa tu na lawama mnataka ziende kwa wengine.poleni sana

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU