Monday, July 23, 2012

YANGA NA APR ZATINGA NUSU FAINALI

 Wachezaji wa Yanga wakifurahia ushindi 
Said Bahanuzi chini katika mishemishe za kusaka mabao

Timu ya Yanga imetinga nusu fainali ya Michuano ya Kombe la Kagame baada ya kuifunga timu ya Mafunzo ya Zanzibar Kwa penati tano Kwa nne katika mchezo uliofanyika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. Dakika tisini za mchezo huo zilipo malizika timu hizo zilikua zimetoka sare ya kufungana bao 1-1  , ndipo zikapigwa penati na yanga kuibuka kidedea. 

Nayo timu ya APR ya Rwanda Imetinga nusu Fainali baada ya kuifunga URA ya Uganda bao 2-1. Hivyo basi timu ya Mafunzo na URA zimeondolewa katika michuano ya Kombe la Kagame. 

Hapo kesho wekundu wa msimbazi watashuka dimbani kucheza na Azam FC katika robo fainali ya michuano ya Kagame mchezo utakao chezwa saa kumi jioni na mchezo wa kwanza utakua saa nane mchana kati ya Atletico ya Burundi na Vita club ya Kongo.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU