Meneja mauzo wa Kinondoni na Ilala wa Kampuni ya Bia Tanzania, Victor Kavishe (wa pili kushoto) akimkabidhi Kikombe nahodha wa Klabu ya Lugalo, Eliutha Shawa mara baada ya kuibuka mabingwa wakati wa mashindano Safari Darts kwa Vilabu vya Mkoa wa Dar es Salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa Darts Mkoa wa Dar es Salaam.
KLABU ya Lugalo ya mchezo wa vishale ya jijini Dar es Salaam, ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya vishale yaliyojulikana kwa “Safari Darts Dar Clubs Championship 2012” kwa kushilikisha vilabu kumi vya mchezo huo vya jijini Dar es Salaam kwa pointi 18 mwishoni mwa wiki.
Lugalo walitwaa ubingwa huo na kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu shilingi laki tatu na Meneja mauzo wa Kinondoni na Ilala, Victor Kavishe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo.
Mshindi wa pili katika mashindano hayo ni klabu ya Upanga ambayo ilipata pointi 16 na wa tatu ni Polisi Balax ambao walipata pointi 13.
Mashindano hayo yaliendeshwa kwa mfumo wa ligi mpaka washindi kupatikana na vilabu vilivyoshiliki ni Lugalo, Upanga,Polisi Balax,Freinds,Magereza,Mbezi Beach,Kashudu,Kawe na Kimanga.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja mauzo wa Kinondoni na Ilala wa TBL, Victor Kavishe alisema kampuni ya Bia ya Safari Lager iko bega kwa began a mchezo wa Darts kuhakikisha inasaidia kwa kila linalowezekana kuendeleza na kukuza mchezo huo hapa nchini na pia aliwapongeza washiriki wote kwa utulivu mpaka washindi kupatika kkwa amani na aliwapongezwa washindi Lugalo kwa kutwaa Ubingwa ambao pia walikuwa washindi wa pili katika mashindano ya mchezo huo ya Afrika mashariki yaliyomalizika hivi karibuni.
Nae katibu wa Darts Mkoa wa Dar es Salaam, Lambarth Rwihula aliishukuru Kampuni ya Bia ya Safari Lager kwa ufadhili wao na kuwaomba makampuni mengine waige mfano huo.
0 maoni:
Post a Comment