Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukingo(kulia) akimkabidhi Kombe
Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa, Asach Togocho kwa ajili ya zawadi ya Bingwa
wa mashindano ya Safari Pool Taifa yanayotarajiwa kuanza Septemba 27-30 mwaka
huu jijini Mwanza.
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza
zawadi kwa klabu bingwa wa mashindano ya Safari Pool Taifa
yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 27–30 mwaka huu jijini
Mwanza kwa kushilikisha mabingwa wa Vilabu kutoka katika mikoa 16.
Akizungumza
na waandishi wa habari Meneja wa Bia ya Safari Lager, Bw. Oscar
Shelukindo alisema zawadi kwa Bingwa wa fainali za Safari Pool Taifa
2012 ni pesa taslimu Shilingi milioni tano(5,000 000), Kikombe na Medali
za dhahabu,ambapo zawadi zingine ni;
ZAWADI NGAZI YA FAINALI TAIFA
ZAWADI KWA TIMU
|
KIASI
|
ZAWADI KWA MMOJA MMOJA
|
KIASI (WANAUME)
|
KIASI (WANAWAKE)
|
Bingwa
|
5,000,000.00
|
Bingwa
|
500,000.00
|
350,000.00
|
Mshindiwapili
|
2,500,000.00
|
Mshindiwapili
|
250,000.00
|
200,000.00
|
Mshindiwatatu
|
1,250,000.00
|
Mshindiwatatu
|
200,000.00
|
150,000.00
|
Mshindiwanne
|
750,000.00
|
Mshindiwanne
|
150,000.00
|
100,000.00
|
4 Losses on 8 Regional’s kilammojaatapata
|
350,000.00
|
4 Losses on best 8 for men and ladies
|
100,000.00
|
50,000.00
|
8 Losses on 16 Team’s kilammojaatapata
|
150,000.00
|
8 Losses on best 16 for men and best 14 for ladies
|
50,000.00
|
30,000.00
|
Safari
Lager imekuwa wadhamini wa mchezo wa Pool toka mwaka 2008, imedhamini
mashindano ya ndani na ya nje ya nchi pia. Imedhamini timu ya Taifa ya
mchezo wa Pool kushiriki mashindano ya dunia ya mchezo wa Pool nchini
Ufaransa mwezi wa kumi mwaka 2010 ambapo timu yetu ilifanya vizuri.
Mashindano ya kimataifa ya mchezo wa Pool yatafanyika katikati ya mwezi
wa kumi nchini Uingereza, katika mji wa Blackpool
Naye
Katibu wa Chama cha Pool Taifa (TAPA), Bw.Amos Kafwinga alivitaja
vilabu vilivyofuzu kushiriki fainali za Taifa jijini Mwanza ambavyo ni
Balele Klabu kutoka mkoa Kagera,Spider kutoka Tanga,Mbosho klabu kutoka
Kilimanjaro,2eyes kutoka Arusha,Janja Wild kutoka Manyala,Sabasaba klabu
kutoka Lindi,Texas klabu kutoka Tabora,New Stand kutoka
Shinyanga,Anatory klabu kutoka Morogoro,Atlantic klabu kutoka
Dodoma,Nginja klabu kutoka Iringa,Blue House kutoka Mbeya,Sun City
kutoka Temeke,Kayumba klabu kutoka Ilala,Meeda kutoka Kinondoni na
wenyeji wa mashindano watawakilishwa na klabu ya Paseansi.
Alisema katibu fainali zinatafanyika katika Hoteli ya Monach jijini Mwanza na tamati ya fainali hizo ni Septemba 30 mwaka huu.
Mwaka
jana mashindano ya taifa yalihusisha timu za mikoa ambapo Mkoa wa
Dodoma waliibuka mabingwa baada ya kuwatoa mkoa wa kimashindano wa
Temeke. Mashindano ya mwaka jana yalifanyika mkoani Dodoma. Timu ya
Dodoma walijipatia kikombe,medali za dhahabu na jumla ya shilingi
milioni tano taslimu lakini mwaka huu mashindano yanahusisha Vilabu
hatujui nani ataibuka bingwa kwani upinzani ni mkubwa sana.
0 maoni:
Post a Comment