Friday, September 21, 2012

TBL KUPITIA KINYWAJI CHAKE CHA KILIMANJARO YAKABIDHI MABASI MAPYA KLABU ZA SIMBA NA YANGA
 Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akicheza sambamba na mashabiki wa timu hiyo wakionesha furaha yako baada ya Kampuni ya Bia Tanzania TBL kuvikabidhi klabu za Simba na Yanga mabasi mapya katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goetzsche  kulia akimkabidhi mfano wa ufunguo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga wakati wa hafla ya kukabidhi basi jipya kwa klabu hiyo. TBL ndio mdhamini Mkuu wa klabu za Simba na Yanga.


 Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akipokea mfano wa ufunguo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goetzsche kama ishara ya makabidhiano ya basi jipya lililotolewa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo


 Viongozi wa Simba na Yanga wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa TBL


Mkuu wa Usambazaji wa TBL, James Bokella akionesha ishara ya kuanza rasmi kwa msafara wa kuyatembeza magari ya Simbana Yanga katika mitaaya jiji la Dar es Salaam ili mashabiki wa timu hizo wayaone.

1 maoni:

shukuru sibonike said...

nachukua nafasi hii kuwapongeza TBL kupitia kinywaji chao cha kilimanjalo, kwa udhamini mnono waloutoa kwa vilabu vyetu, na hii iwe changamoto kwa vilabu hivi viwili kufanya vema katika michezo yao yote ya kitaifa na kimataifa kwani TBL imeonesha juwajali na kuwaweka uptodate kama dunia ya sasa inavotaka.

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU