Wagombea
13 kati ya 15 waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye
Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) wamepitishwa baada
ya usaili uliofanyika juzi.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala,
waliopitishwa kwenye nafasi ya uenyekiti ni Isabellah Huseein Kapera,
Joan Ndaambuyo Minja na Lina Paul Kessy.
Makamu
Mwenyekiti ni Rose Kisiwa wakati wanaowania nafasi ya Katibu Mkuu ni
Amina Ali Karuma na Cecilia Oreste Makafu. Mgombea pekee wa nafasi ya
Katibu Msaidizi, Macky Righton Mhango naye amepita kwenye usaili huo.
Aliyepitishwa kwenye nafasi ya Mhazini ni Rose Stewart Msamila.
Furaha
Francis na Zena Chande wamepitishwa kuwania nafasi ya Mjumbe wa Mkutano
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakati waliopita
kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TWFA ni Triphonia Ludovick
Temba, Rahim Salum Maguza na Sophia James Charles.
Hivi
mchakato wa uchaguzi wa TWFA uko katika kipindi cha kukata rufani
ambapo ni kuanzia Oktoba 15-17 mwaka huu. Rufani zinatakiwa zifike kwa
Katibu Mkuu wa TFF kabla ya saa 10 kamili jioni ya Oktoba 17 mwaka huu.
Wagombea wawili ambao hawakupitishwa kwa ajili ya uchaguzi huo
unaotarajiwa
kufanyika Novemba 4 mwaka huu ni Julliet Mndeme na Jasmin Soud
walioomba ujumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF. Wagombea hao ambao pia walikuwa
wamewekewa pingamizi hawakufika kwenye usaili.
PONGEZI KWA UONGOZI MPYA ARFA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) uliochaguliwa katika
uchaguzi uliofanyika jana (Oktoba 14 mwaka huu).
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa COREFA walivyo na imani kubwa kwao katika
kusimamia mchezo huo mkoani Pwani.
TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya COREFA
chini ya uenyekiti wa Hassan Othman Hassan ambaye amechaguliwa tena
kuongoza chama hicho.
Uongozi
huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha
shughuli za mpira wa miguu mkoani Pwani kwa kuzingatia katiba ya COREFA
pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya COREFA na Kamati ya Uchaguzi
ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za
uchaguzi za wanachama wa TFF.
Viongozi
waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni Hassan Othman Hassan
(Mwenyekiti), Riziki Majala (Katibu), Geofrey Irick Nyange (Mjumbe wa
Mkutano Mkuu TFF), Juma Haruna Kisoma (Mwakilishi wa Klabu TFF) na
Abubakar Allawi (Mhazini).
Waliochaguliwa kuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji katika uchaguzi huo uliofanyika kisiwani Mafia ni Musa Bakari Athumani, Godfrey Magnus Haule na Gwamaka Oden Mlagila. Mwakilishi wa Wanawake ni Florence Ambonisye.
0 maoni:
Post a Comment