HATIMAYE
mashabiki sita wakaochuana ili kupata wawili kupitia shindano la kusaka mashabiki
bora wa Ligi Kuu ya England, maarufu zaidi kwa jina la ‘Castle Lager Superfans’,
wamejulikana.
Washindi hao
sita wamepatikana kutokana na mchujo mkali kutoka kwa mashabiki 361
waliojitokeza kushiriki shindano hilo linaloendeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL), kupitia kinywaji chake cha Castle Lager.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Bia ya Castle Lager,
Kabula Nshimo alisema ilikuwa ni mchujo mgumu, kutokana na wingi wa mashabiki
waliojitokeza.
Kabula alisema,
miongoni mwa hao sita, watapatikana wawili ambao ndio watakaoungana na
mashabiki kutoka nchi nyingine kuunda timu ya ushangiliaji katika fainali za
Kombe la Mataifa Afrika, zitakazofanyika Afrika Kusini mwakani.
Aliwataja
mashabiki hao sita na mikoa wanayotoka ikiwa kwenye mabano kuwa ni, Stephen
Chuma , John Mosha, Filbert Nestory (Dar es Salaam), Charles Mbaza (Arusha),
Denis Mlowe (Iringa) na Yahaya Hamza (Mwanza).
Castle Lager
ambao pia ni wadhamini wenza wa Ligi Kuu ya England, itawatembeza mashabiki hao
mikoa yote ili kuomba kura, pia kupitia promosheni mbalimbali zitakazoendeshwa
nchi nzima.
Kabula alisema,
mashabiki 361 walijitokeza kwa kutuma picha zao katika mtandao wa kijamii wa
Facebook na promosheni walizoziendesha katika mikoa mbalimbali.
Meneja huyo
alisema, baada ya mchujo walipatikana washindi 32 kutoka mikoa ya Dar es
Salaam, Mbeya, Iringa, Shinyanga, Mwanza, Arusha na Kilimanjaro, ambao
walipigiwa kura na kupatikana 15.
“Katika hao 15
ndio ambao walifanyiwa mahojiano ya ana kwa ana, hivyo wamechujwa na kupatikana
sita, ambapo watasakwa washindi wawili ili waunde timu ya Castle Lager
Superfans Tanzania,” alisema.
Kabula alisema
washindi hao wawili watakaopatikana, wataungana na wengine kutoka Swaziland,
Zambia, Afrika Kusini na Zimbabwe ili kuunda timu ya ushangiliaji
itakayogharamiwa kila kitu katika fainali za Kombe la Mataifa Afrika hapo
mwakani. Fainali hizo zitafanyika Afrika Kusini.
Mashabiki hao
sita unaweza kuwapigia kura kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno ukitaja jina la
mshiriki kwenda namba 0683 536631.
0 maoni:
Post a Comment