Shirikisho la Ngumi za Kulipwa la Afrika ya
Mashariki na Kati (ECAPBA) limempongeza bondia Mtanzania Thomas Mashali
kwa kushinda ubingwa wa ECAPBA katika uzito wa kati (middleweight)
uliokuwa wazi jana tarehe 14 Octoba.
Mpambano
huo uliomkutanisha Thomas Mashali na Sebyala Med toka Uganda na
ulifanyika katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese katika wilaya ya
Kinondoni na kuhudhuriwa na maelfu ya Watanzania pamoja na wageni toka
nchi jirani.
ECAPBA
inatambua na kuenzi kipaji alichoonyesha bondia Thomas Mashali na
kumtakia kila la kheri katika maisha yake kama bingwa halali wa ECAPBA.
Mpambano huo uliandaliwa na
promota Seleman Simunyu na kusimamiwa kwa ushirikiano wa pamoja kati
ya TPBC na TPBO. Kamishna wa mpambano alikuwa ni Boniface Wambura ambaye
ni Mwenyekiti wa Kamati ya Viwango na Ubingwa wa TPBC, refarii alikuwa
Nemes Kavishe ambaye ndiye Katibu Mkuu wa TPBC, Jaji namba 1 alikuwa
Mark Hatia wa TPBC, Jaji namna 2 alikuwa aid Chaku ambaye ni Katibu Mkuu
Msaidizi wa TPBO na jaji namba 3 alikuwa Sake Mtulya wa TPBO.
Bingwa Thomas Mashali anatakiwa akae na ubigwa huo kwa kipindi cha miezi sita na kuutetea kabla kipindi hicho hakijamalizika.
Aidha ECAPBA linampongeza Rais wa
TPBO Yasin Abdallah (Ustaadh) kwa kazi nzuri aliyofanya kusimamia
utaratibu mzima wa mpambano huo!
Shirikisho la Nguni za Kulipwa la Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA)
lina wanachama toka nchi zifuatazo: anzania, Kenya, Uganda, Sudan ya
Kusini, Ethiopia, Malawi, Rwanda, Burundi, DRC Congo na Zambia.
0 maoni:
Post a Comment