Mshindi wa Redd's Miss Talent 2012,Babylove Kalala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na warembo wengine walioingia hatua ya tano bora ya Redd's Talent iliyofanyika usiku huu katika hoteli ya Gireffe,jijini Dar es salaam.Kutoka kulia ni Mshiriki namba 13 kutoka kanda ya Mashariki,Joyce Baluhi,Mshiriki namba 15 kutoka Temeke,Catherine Masumbigana,Mshiriki kutoka Kanda ya Mashariki,Irene Verda na Mshiriki namba 26 kutoka Kinondoni,Brigit Alfred.
MREMBO kutoka
Kagera anayewakilisha Kanda ya Ziwa katika shindano la Redd’s Miss Tanzania,
Babylove Kalala juzi usiku alifanikiwa kutwaa taji la Redd’s Miss Talet
lililofanyika kwenye hoteli ya Giraffe, iliyopo Kunduchi, Dar es Salaam.
Kutokana na
ushindi huo, Babylove sasa anaunga na Miss Photogenic, Lucy Stephano na Redd's
Miss Tanzania Sports Lady, Mary Chizi kuingia hatua ya 15 ya Redd’s Miss
Tanzania litakalofanyika mwishoni mwa wiki.
Babylove
alifanikiwa kuwashinda warembo wengine 30 aliokuwa anachuana nao, baada ya
kuonesha kipaji cha hali ya juu wakati akicheza ngoma kwa kutumia nyoka, kiumbe
ambaye warembo wengine walionekana kumuogopa mno.
Warembo wengine
waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora walikuwa ni Joyce Baluhi na Irene
Verda wa Kanda ya Mashariki, Catherine Masumbigana (Temeke) na Brigit Alfred
(Kinondoni).
Mgeni rasmi
katika shindano hilo alikuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Catherine Magige ambaye
aliwataka warembo wanaoshiriki kutumia mashindano hayo kama chachu ya kufikia
malengo waliyojiwekea.
Akizungumza
mara baada ya kutwaa taji hilo, Babylove aliwashukuru washiriki wengine kwa
kuwa chachu ya yeye kuhakikisha anakuwa mbunifu zaidi, huku akiahidi kufanya
makubwa katika shindano la Redd’s Miss Tanzania.
Shindano la
Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original
kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
0 maoni:
Post a Comment