Bondia
Thomas mashali wa Tanzania na Mganda Medi Sebyala wanatarajiwa kupima
uzito Jumamosi saa nne asubuhi katika ukumbi wa Friends Corner manzese
tayari kwa mpambano wao utakaofanyika oktoba 14 Jijini Dar es salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mratibu wa mpambano huo unaosimamiwa na
oganaizesheni ya Ngumi za kulipwa nchini TPBO Regina Gwae alisema
upimaji huo ndo hatua ya mwisho kuelekea kujua nani atanyakua ubingwa wa
Afrika Mashariki na kati.
Alisema mbali na mabondia hao pia mabondia wa mapambano ya utangulizi ambapo Abdul Awilo atapambana na Shedrack Juma, selemani shaaban atapambana na Hamisi Mohamed Jonas Segu atapambana na Ibrahim Class wkati Charles mashali atapambana na Teacher Aron nao watapima.
Alisema
maandalizo yote yamekamilika ikiwemo waamuzi wenye sifa za kuchezesha
mapambano ya kimataifa wameshapatikana na majina yao yatatangazwa
jumamosi.
Mgeni rasmi katika pambano hilo ni
Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Charles Kenyela ambaye anatarajiwa kuambatana na wageni wengine maalum wakiwemo wabunge.
Alisema
anashukuru kwa ushirikiano wa viongozi katika maandalizi na hatimaye
maandalizi yanaelekea ukingoni na pambanolinatarajiwa kuvuta hisia za
watu wengi na wapenzi wa ngumi jijini Dar es Salaam.
Regina
alishukuru kampuni ya Promasidor wasambazaji wa SOSSI Poa, Gazeti la
Jambo leo,City Sports Lounge na Times Fm kwa kuwa bega kwa bega
kuhakikisha pamnano hili linafanikiwa na kusema milango bado iko wazi
kwa wadau kujitokeza kufanikisha mchezo huo ambao ni chanzo cha ajira
kwa vijana.
0 maoni:
Post a Comment