Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea kesho (Oktoba 13 mwaka huu) kwa timu
kumi kupambana kwenye viwanja vitano tofauti katika raundi ya saba ya
ligi hiyo yenye timu 14.
Polisi
Morogoro itaikaribisha Azam kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro
wakati mwamuzi wa FIFA, Oden Mbaga atakuwa Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine jijini Mbeya kuchezesha mechi kati ya wenyeji Tanzania Prisons
na Oljoro JKT.
Jijini
Tanga, Simba itakuwa mgeni wa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani
katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Simon Mberwa kutoka Pwani
akisaidiwa na Godfrey Kihwili na Abdallah Uhako wote kutoka Arusha.
Mechi
nyingine za kesho ni Ruvu Shooting dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja
wa Mabatini mjini Mlandizi, na Mtibwa Sugar watacheza na Mgambo Shooting
kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Wakati
huo huo, Azam imeomba mechi zake za nyumbani dhidi ya Yanga na Simba
zichezwe kwenye uwanja wake wa Azam Complex ulioko Chamazi badala ya
Uwanja wa Taifa.
Nayo
Ruvu Shooting imeomba mechi yake ya ugenini dhidi ya Yanga ya Oktoba 20
mwaka huu ichezwe Uwanja wa Taifa badala ya Uwanja wa Azam Complex.
Maombi
hayo yatawasilishwa kwenye kikao cha Kamati ya Ligi ya TFF
kinachotarajiwa kufanyika kesho (Oktoba 13 mwaka huu) kwa ajili ya
kufanyiwa uamuzi.
0 maoni:
Post a Comment