MShiriki wa Redds Miss Tanzania 2012, Babylove Kalala akijarimu kumuuma nyoka wakati mrembo huyo pamoja na wenzake wanaowania taji hilo walipotembelea eneo la Snake Pak mjini Arusha.
Warembo
wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2012 jana walitembelea eneo la
Utalii la ufugaji nyoka la jijini Arusha maarufu kama ARUSHA SNAKE PARK
na kujionea nyoka wa aina mbalimbali, Mamba, Kenge, ndege aina ya
Bundi, Tai na Tumbiri.
Warembo
hao ambao wapo katika ziara ya kutembelea Mikoa ya Kanda ya Kaskazini
kwaajili ya kujionea vivutio mbalimbali vya Utalii nchini na kujifunza
mambo tofauti tofauti.
Pamoja
na kujionea Nyoka hao na kucheza nao kwa kuwa vaa shingoni pia warembo
hao walipata fursa ya kujifunza juu ya tamaduni za Mila ya Wamaasai na
kutembelea vibanda vya urembo wa Kimasai.
Mrembo wa Kilimanjaro, Anande Raphael (kushoto) akipozi na Mrembo wa Lindi, Irine Veda huku wakiwa na nyoka.
Mrembo Diana Hussein nae aliweka mapozi yake na nyoka
Warembo wakimwangalia Catherine Masumbigana aliyemzungusha nyoka shingoni
Hapa ni Mrembo wa Kitongoji cha Ukonga jijini Dar es Salaam, Mary Chizi akila pozi.
Jesca Haule mrembo kutoka Kitongoji cha Chang'ombe jijini Dar es Salaam nae alionesha ujasiri wake wa kumvaa nyoka.
Wapo walio ogopa kama Miss Photogenic 2012, Lucy Stephano
Mrembo wa Mbeya Caren Elias nae aliogopa sana. Kulia ni Noela Michael kutoka Tabata nae akiogopa hata nyoka hajamshika.
Lightness Michael nae aliweka pozi na Nyoka
Warembo wakiwa katika eneo la Historia ya Jamii ya wamaasai ambayo nayo ipo Meserani mjini Arusha.
Mrembo wa Pwani, Rose Lucas akipita katika sehemu ya Historia ya Wamasai.
Miss Tanzania 2011, Salha Izrael nae akitoka katika vibanda vya biashara
Elizabeth Diamond mrembo kutoka Singida akiangalia shanga na urembo za aina mbalimbali kwaajili ya kununua.
Mrembo wa Kahama Mkoani Shinyanga, Happiness Rweyemamu nae alikuwa akitafuta cha kununua.
Mkuu wa Itifaki ya Miss Tanzania, Albert Makoye akipiga picha na warembo wa Miss Tanzania akiwa amevalia vazi rasmi la Kabila la Kimasai.
Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, Albert Makoye na Mrembo Joyce Baluhi wakiwa wamevalia mavazi rasmi ya jamii ya Wamaasai.
WAREMBO
wanaoshiriki kuwania taji la Redd’s Miss Tanzania leo usiku wanatarajiwa
kupanda jukwaani kumsaka Miss Top Model, katika shindano linalotarajiwa
kufanyika hoteli ya Naura Spring, mjini hapa.
Mrembo
atakayefanikiwa kutwaa taji hilo moja kwa moja ataingia katika 15 bora ya
Redd’s Miss Tanzania, shindano linalotarajiwa kufanyika Novemba 3, mwaka huu.
Mpaka sasa Miss
Mbulu, Lucy Stephano amejihakikishia kuingia katika hatua hiyo, baada ya
kufanikiwa kutwaa taji la Miss Photogenic, lililofanyika Monduli mwishoni mwa
wiki.
Akizungumza na
gazeti hili mjini hapa jana, Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania, Haidan
Ricco alisema kila kitu kipo tayari n kinachosubiriwa ni kujua nani atatwaa
taji hilo.
“Warembo wote
wako sawa na wamejiandaa vema kuhakikisha wanatoa upinzani mkubwa, naamini
mashabiki watakaohudhuria watapata burudani ya aina yake,” alisema.
Ricco alisema,
baada ya shindano hilo warembo wote wanatarajiwa kuondoka mjini hapa kesho
asubuhi kuelekea Tanga kwa ajili ya kutembelea mapango ya Amboni, kabla ya
kurejea Dar es Salaam.
Warembo wapatao
30 wanawania taji la Redd’s Miss Tanzania, ambalo kwa sasa linadhaminiwa na
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.
0 maoni:
Post a Comment