Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewarejesha nyumbani
waamuzi wasaizidi wanne waliokuwa wameteuliwa kuchezesha fainali za Nane
za Afrika kwa Wanawake (AWC) zinazoanza kesho (Oktoba 28 mwaka huu
jijini Malabo, Equatorial Guinea.
Kwa mujibu wa Meneja wa Waamuzi wa CAF, Bester Kalombo waamuzi hao
wamerejeshwa nyumbani baada ya kushindwa mtihani wa utimamu wa mwili
(physical fitness test) uliofanyika jana (Oktoba 26 mwaka huu).
Waamuzi hao ni Emmanuella Aglago kutoka Ghana, Atallah Mona Mahmoud
wa Misri, Mary Njoroge (Kenya) na Nchama Edu Manuela wa Equatorial
Guinea.
Kalombo alisema baada ya hao kuondolewa wameongeza waamuzi
wasaidizi wengine wawili ili kuziba nafasi zao. Waamuzi wasaidizi
walioongezwa ambao walikuwa kwenye orodha ya akiba ni Marthe Sakobo
kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Mercy Zulu wa Zambia.
Waamuzi wa kati walioteuliwa kuchezesha fainali hizo na ambao wote
walifaulu mtihani huo ni Aissatta Amegee (Togo), Christine Ziga (Ghana),
Gladys Lengwe (Zambia), Grace Msiska (Malawi), Incaf El Harkaoui
(Morocco), Kankou Coulibaly (Mali), Ledia Tafese (Ethiopia), Maximina
Luzia Bernado (Angola), Nabikko Ssemambo (Uganda), Naema Rashad Mohamed
(Misri) na Therese Sagno (Guinea).
Kwa upande wa waamuzi wasaidizi waliofuzu ni Adijat Bosede Momo,
Bernadettar Kwimbira (Malawi), Botsalo Watlala Mosimane (Botswana),
Diana Junia Mukasa (Uganda), Lidwine Rakotozafinoro (Madagascar), Mana
Ayawa Dzodope (Togo), Marthe Gamoeda Laconte (Jamhuri ya Afrika ya
Kati), N’dah Francois Tempa (Benin), Souad Oulhaj (Morocco), Trhas
Gebreyohanis (Ethiopia) na Tseke Ngouono (Congo Brazzaville).
0 maoni:
Post a Comment