Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na
Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwa kenye picha ya pamoja na
Warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Tanzania 2012 pamoja na Viongozi
wa Kamati ya Miss Tanzania.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akisalimia na Msimamizi (Matron) wa warembo wa Redd's Miss Tanzania
2012,Irene Karugaba wakati Warembo hao walipotembelea Nyumbani kwa
Waziri Mkuu Mstaafu,Monduli ili Kupata Baraka zake.Mh. Lowassa
aliwapokea
warembo hao kwa furaha na kuzungumza nao machache juu ya mafanikio ya
Mashindano hayo na Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa akizungumza na Warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Tanzania
2012 waliofika nyumbani kwake Monduli leo na kupata wasaa kwa kuzungumza
nae mambo mawili matatu juu ya mafanikio ya Mashindano hayo na
Maendeleo ya Taifa letu kwa ujumla.
0 maoni:
Post a Comment