Katibu mtendaji wa BASATA Ghonche materego
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewaagiza viongozi wa Mashirikisho ya sanaa hapa nchini kufuatilia kwa karibu matukio ya ukiukwaji wa maadili yanayoendelea katika Sanaa hivi sasa na kuchukua hatua kwa wnaobainika kufanya hivyo.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewaagiza viongozi wa Mashirikisho ya sanaa hapa nchini kufuatilia kwa karibu matukio ya ukiukwaji wa maadili yanayoendelea katika Sanaa hivi sasa na kuchukua hatua kwa wnaobainika kufanya hivyo.
Katibu
Mtendaji wa BASATA Ghonche Materego,
mbali na BASATA kuwakemea vikali wasanii wanaotumia majukwaa kwa
kuidhalilisha Sanaa wao wenyewe na watazamaji pia limeyataka mshirikisho kushirikiana
na vyama vyao kuwaita wale wote watakaohusika na uvunjwaji wa maadili ili kuwakanya
katika hatua ya kwanza na kama wasipoacha tabia hizo Baraza litawafungia
kujishughulisha na kazi ya Sanaa hapa
nchini.
“Shirikisho
la Muziki tumeliagiza kuangalia tungo za wanamuziki zenye maneno yenye lugha
isiyofaa, Shirikisho la Sanaa za Ufundi limeagizwa kuwachukulia hatua wasanii
wachoraji na wachongaji wanaotengeneza Sanaa zinazokiuka maadili. Aidha
Shirikisho la Sanaa za Maonyesho waliagizwa kufuatilia wasanii wote wanaocheza
bila staha majukwaani. Na mwisho Shirikisho la Filamu tumeliagiza kuwaita,
kuwaonya na kuwachukulia hatua wasanii wote katika fani ya Filamu wanaovaa nusu
utupu bila kuzingatia husika katika kazi za Sanaa,” amesema Ghonche.
Aidha
Baraza limewaagiza wamiliki wa kumbi zote za burudani kuzingatia maadili pale
ambapo Sanaa zitakuwepo jukwaani na kwamba baraza halitasita kuufungia ukumbi
wowote utakaokiuka agizo hilo.
“Pia
tunaviomba vyombo vya usalama kuhakiki muda wa vibali vya maonyesho na bila
kuchelewa kuwachukulia hatua stahiki wasiozingatia muda wa maonyesho. Na tunawakumbusha
wamiliki wa vyombo vya Habari na Wahariri kuunga mkono juhudi zinazofanywa na
wasimamizi wa sanaa kwa kutokurusha wala kutangaza maonyesho ambayo kwa njia
yoyote yanachangia mmomonyoko wa maadili ya Taifa letu,” alisema Ghinche.
Kwa suala hili, Baraza linaziomba mamlaka
zinazohusika na usimamizi wa uendeshaji wa vyombo vya habari nchini kuingilia
kati na kuvichukulia hatua vyombo vya habari ambavyo kila siku vimekuwa mstari
wa mbele kueneza wimbi la mmomonyoko wa maadili hapa nchini na kushusha hadhi
ya Tasnia/Sekta ya Sanaa nchini.
0 maoni:
Post a Comment