Mbuyu Twite aliyeenda juu (nyuma) kuokoa kwa kichwa
YANGA iliyokuwa na mwanzo mbaya wa
msimu, hatimaye imeifikia Simba kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya
Tanzania Bara kufuatia ushindi wa 3-0 dhidi ya Mgambo JKT, huku Wekundu
wa Msimbazi waking'ang'aniwa kwa sare ya 1-1 dhidi ya timu ya mkiani ya
Polisi kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jioni ya leo.
Ushindi huo unamaanisha kwamba Yanga sasa imelingana pointi 23 na Simba kileleni baada ya mechi 11. Hata hivyo, Simba yenye wastani wa magoli 12, inaendelea kuongoza ligi kwa wastani wa goli moja zaidi ya Yanga yenye wastani wa magoli 11. Simba imefunga magoli 20 na kufungwa 8 wakati Yanga imefunga magoli 21 na kufungwa 10.
Yanga ilianza kuhesabu goli la kwanza katika dakika ya pili tu ya mchezo kupitia kwa beki wake wa kati Nadir Haroub 'Cannavaro' aliyefunga kwa kichwa kufuatia mpira wa 'fri-kiki' uliopigwa na kiungo Haruna Niyonzima.
Washambuliaji Didier Kavumbagu na Jerry Tegete wakaongeza mengine mawili wakati Yanga ilipopata ushindi wa saba katika mechi 11 na kuwasahaulisha mashabiki wao mwanzo mbaya wa msimu uliowafanya wamfukuze kocha Mbelgiji Tom Saintfiet aliyedumu nao kwa siku 80 tu huku akiwa ameshawapa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).
Mambo hayakuwa mazuri kwa mabingwa Simba ambao walitanguliwa kwa goli la dakika ya 33 kutoka kwa Mokili Lambo, aliyekuwa ameingia uwanjani dakika 5 tu zilizopita kuchukua nafasi ya John Bosco aliyepumzishwa katika dakika ya 28.
Simba walirejea kipindi cha pili wakiwa nyuma kwa goli 1-0 kabla ya kiungo wao aliye katika kiwango cha juu tangu kuanza kwa msimu huu Amri Kiemba kuwasazishia katika dakika ya 57 akimalizia kona iliyochongwa na Emmanuel Okwi.
Ilikuwa ni sare ya 5 katika mechi 7 zilizopita za Simba baada ya kushinda zote nne za kwanza mfululizo, wakati Polisi ilipata pointi yao ya tatu kutokana na sare tatu huku ikiendelea kubaki mkiani mwa ligi ikiwa haina ushindi baada ya mechi 11. Imefungwa mechi 8.
Sare nyingine katika mechi za ugenini, ilionekana kumchanganya kocha wa Simba, Mserbia Milovan Cirkovic ambaye alidai kwamba refa Jacob Ondongo kutoka Mara alichezesha vibaya na kwamba alionekana kuipendelea timu ya mwenyeji.
Kocha msaidizi wa Polisi, Ally Jangalu aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri akisema walikuwa na makosa katika upande wa ufungaji lakini wamerekebisha kiwango tangu walipocheza dhidi ya Ruvu Shootings ambapo walilala 2-1 kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.
Kwenye Uwanja wa Taifa leo, Mgambo ambao waliwashikilia Simba katika sare ya kustusha mkoani Tanga iliyochangia kiungo wa Wekundu, Haruna Moshi 'Boban' kusimamishwa, walijikuta wakimaliza wakiwa 10 uwanjani baada ya beki wao Salum Mlima kumchezea rafu beki wa Yanga, Mbuyu Twite katika dakika ya 85 na kutolewa kwa kadi nyekundu na mwamuzi Martin Saanya wa Morogoro.
Coastal Union ya Tanga iliyo katika nafasi ya tatu itajaribu kuitetea nafasi yake wakati itakapocheza ugenini dhidi ya Azam iliyo katika nafasi ya nne kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi kesho.

0 maoni:
Post a Comment