Msanii wa kikundi cha ngoma cha Bujora akichezea nyoka kwa kuingiza
kichwa mdomoni wakati wakitumbuiza watu waliofika kushuhudia mashindano
ya mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) yaliyofanyika Mwaloni Mkoani
Mwanza jana.
Mabingwa wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) Mkoani Mwanza upande wa wanawake timu ya Wanawake na Maendeleo kutoka Misungwi wakiwa hawaamini kama wameweza kushinda kwa kuwaacha mbali wenzao na kuwa mabingwa wa mkoa huo na kukabidhiwa jumla ya shilingi laki saba (700,000) kama zawadi ya ushindi wa kwanza.
Wapiga makasia 15 wakinyosha makasia yao juu kabla ya
kuanza kwa fainali za mashindano ya mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat
Race) yaliyofanyika jijini Mwanza jana.
Mabingwa wa ngoma za asili wa mashindano ya ngoma ya kanda ya ziwa
kikundi cha Bujora wakitumbuiza mashabiki wa mashindano ya mitumbwi
yaliyofanyika jana kwenye fukwe za Mwaloni Mkoani Mwanza jana ambapo
washindi watakao wakilisha mkoa huo kwenye fainali wamepatikana.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL akiteta jambo na Afisa Utamaduni na Michezo wa Manispaa ya Ilemela wakati wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) Yaliyofanyika jana Mkoani Mwanza.
Mabingwa wa Mkoa wa Mwanza wa Mashindano ya Mitumbwi ya Balimi
(Balimi Boat Race) timu ya Cheka na Wengi kutoka Misungwi wakiwasili
ufukweni baada ya kuongoza mbio hizo muda wote huku wanaofuatia
wakipishana kwa sekunde tu.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL Fimbo Butallah,
akimuelekeza jambo Nahodha wa timu ya Wanawake na Maendeleo ya Misungwi
Tabu Daudi, ambao ndio washindi wa kwanza kwa upande wa
wanawake Mkoa wa Mwanza mara baada ya kukabidhiwa zawadi yao ya ushindi
wa kwanza kitita cha shilingi laki saba (700,000).
0 maoni:
Post a Comment