Meneja wa Airtel Kanda za Nyanda za Juu
Kusini, Beda Kinunda akizungumza mara baada ya kukabidhi vitabu vya
masomo ya Sayansi kwa shule nne Kiponzelo, Wasa, Mgawa and Lyandembela za jimbo la Kalenga mkoani Iringa.
Meneja Mawasiliano wa Airtel Kanda, Jackson
Mbando (kulia) akimkabidhi kwa Diwani wa Viti Maalum CCM, Vumilia
Mwenda, Tarafa ya Kiponzero, Ifunda Mkoani Iringa. Wanaoshuhudia
makabidhian o hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki ni Katibu wa Mbunge
wa Kalenga, Martin. Airttel ilitoa msaada huo wa vitabu kwa shule nne za
jimbo la Kalenga mkoani Iringa.
Meneja wa Airtel Kanda za Nyanda za Juu
Kusini, Beda Kinunda (kulia) akimkabidhi vitabu vya masomo ya Sayansi
Katibu wa Mbunge wa Kalenga, Martin Simangwa Airtel ilitoa msaada huo wa
vitabu kwa shule nne za jimbo la Kalenga mkoani Iringa.
Meneja wa Airtel Kanda za Nyanda za Juu
Kusini, Beda Kinunda (kulia) akimkabidhi vitabu kwa Mkuu wa shule ya
Sekondari Mgama iliyopo Ifunda Mkoani Iringa, Simeon Lihuluku.
Wanaoshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki ni
Katibu wa Mbunge wa Kalenga, Martin Simangwa (wapilki kulia) na Diwani
wa Viti Maalum CCM, Vumilia Mwenda. Airttel ilitoa msaada huo wa vitabu
kwa shule nne za jimbo la Kalenga mkoani Iringa.
Meneja wa Airtel Kanda za Nyanda za Juu
Kusini, Beda Kinunda (kulia) akimkabidhi vitabu kwa Mkuu wa shule ya
Sekondari Lyandembela iliyopo Ifunda Mkoani Iringa, Adrian Nyakunga.
Wanaoshuhudia makabidhian o hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki ni
Katibu wa Mbunge wa Kalenga, Martin Simangwa (wapilki kulia) na Diwani
wa Viti Maalum CCM, Vumilia Mwenda. Airttel ilitoa msaada huo wa vitabu
kwa shule nne za jimbo la Kalenga mkoani Iringa.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lyandembela
iliyopo Ifunda mkoani Iringa, wakisaidiwa na Meneja Mahusiano wa Airtel
Jackson Mbando (kushoto) kushusha vitabu vya masomo ya Sayansi na
Hisabati vilivyogawiwa katika Shule nne katika jimbo la Kalenga Mkoani
Iringa mwishoni mwa wiki.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lyandembela
iliyopo Ifunda mkoani Iringa, wakionesha vitabu vya masomo ya Sayansi
na Hisabati vilivyogawiwa katika Shule nne katika jimbo la Kalenga
Mkoani Iringa mwishoni mwa wiki na kampuni ya Simu za Mkononi ya
Airtel.Kulia ni Diwani wa Viti Maalum Vumilia Mwenda
Meneja wa Airtel Kanda za Nyanda za Juu
Kusini, Beda Kinunda (kulia) akimkabidhi vitabu kwa Mkuu wa shule ya
Sekondari Wasa iliyopo Ifunda Mkoani Iringa, David Mpalanzi.
Wanaoshuhudia makabidhian o hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki ni
Katibu wa Mbunge wa Kalenga, Martin Simangwa (wapilki kulia) na Diwani
wa Viti Maalum CCM, Vumilia Mwenda. Airtel ilitoa msaada huo wa vitabu
kwa shule nne za jimbo la Kalenga mkoani Iringa.
Shule4 za sekondari mkoani Iringa za faidi na msaad huo
Katika
kuhakikisha kiwango cha elimu nchini kinainuka, kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel chini ya mpango wake wa Shule yetu imeendelea kutoa
msaada wa vitabu kwa shule mbalimbali za sekondari ambapo mwisho mwa
wiki hii Airtel ilitoa vitabu kwa shule za sekondari Kiponzelo, Wasa,
Mgawa and Lyandembela zilizoko mkoani Iring.
Akiongea
wakati wa halfa ya kukabidhi vitabu iliyofanyika katika shule ya
sekondari lyandembela Diwani wa Viti Maalum CCM, Vumilia Mwenda, Tarafa
ya Kiponzero, Ifunda Mkoani Iringa alisema “Tunashukuru Airtel kwa kutoa
haki sawa kwa shule zote nchini kwa kuchangua shule kupitia droo ambayo
imeweza kuwafikia wanafunzi wa shule za Iringa hadi vijijini.
Tumefurahi sana kupata vitabu mbalimbali kwani shule ya sekondari za
hapa Ifunda zina changamoto ya upungufu wa vitabu hasa vya
sayansi na kulifanya somo hilo kuwa na wanafunzi wa chache, lakini hivi
sasa kutokana na msaada wa vitabu vilivyo tolewa vitaongeza ufaulu kwa
wanafunzi wetu”.
Nachukua
fulsa hii kuwaasa wanafunzi wavitumie vitabu hivi vizuri na kujiunga na
masomo ya sayansi, tunaamini vitabu hivi vitaleta ufanisi pamoja na
kuwa na changamoto ya walimu naahidi kuwashirikisha wizara ya elimu ili
kuongeza idadi ya walimu wa sayansi na kuongeza ufaulu zaidi” aliongeza
Bi Mwenda
Naye Mwalimu mkuu wa sekondari ya Wasa David Mpalanzi Iliyoko Wilaya Mfindi Mkoa wa Iringa akiongea kwa niaba ya wakuu wa sekondari wa shule za Mgama, Lyandembela and Kiponzelo
alitoa shukurani kwa Airtel na kusema msaada huo wa vitabu utaweza kuwa
saidia wanafunzi kuwa na uweza wa kujisomea zaidi na kuwawezesha
kufaulu hadi kwenda chuo kikuu ,kwani hapo awali kulikuwa na changamoto
kubwa katika shule zetu ambapo uwiano ulikuwa kitabu kimoja wanafunzi 15
hadi 20. Lakini msaada huu utapunguza zaidi, kwa kweli huu ni msaada
mkubwa katika kuboresha taaluma na kuinua ufaulu hivyo tunaomba program
hii ya shule yetu iendelee ili kuwafikiwa watu wengi zaidi
Tunaomba
Airtel muongeze wigo wa kutoa misaada mbalimbali ya kuboresha elimu na
mazingira kwa ujumla ikiwemo , kutoa komputa, kusaidia upatikanaji wa
maji, na mengine mengi.
Akiongea kwa niaba ya wanafunzi Kaka Mkuu wa shule ya Lyandembela sekondari Taifa Malata
ametoa
shukurani kwa niaba ya wenzao huku akibainisha wanafunzi wengi walikuwa
wakifeli katika masomo mbali mbali kutokana na ukosefu wa vitabu
,wanafunzi hao wameomba uongozi wa Airtel kuwafikirili kutatua
changamoto zingine kama ukosefu wa maji, pamoja na kuwajengea maktaba ya
kuwatosheleza ili kujisomea kwa nafasi zaidi
Akiongea
kwa niaba ya Airtel Meneja mauzo wa Airtel Beda Kinunda amewataka
wanafunzi wa sekondari zote mkoani Iringa kuongeza uwezo wa kujisomea
ili Airtel ione ufaulu wa wanafunzi unaongezeka kupitia msaada unatolewa
na Airtel, pia natoa wito vitabu hivi vitunzwe ili viweze
kuwafaidisha wanafunzi wengi kwa kuwa Airtel imeanzisha mpango wa
Airtel Shule yetu ili iwe chachu kukuza Elimu.
Airtel
imeanzisha mpango wa Airtel Shule yetu ili kuendeleza Elimu Inchini
Tanzania Umeanzisha Mpango huo na kuweza kushindanisha shule mbalimbali
zaidi shule 3000 na shule zinazo shinda hupewa vitabu katika bahati na
sibu hiyo. shule NNE za mkoa wa Iringa zilibahatika kushinda.
0 maoni:
Post a Comment