Kavumbangu akimfunga kipa wa Azam, Mwadini Ali
YANGA SC imepanda kileleni mwa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuifunga Azam FC mabao 2-0 kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Yanga iongoze
Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 26, ikiwa imebakiza mechi moja ya mzunguko wa
kwanza dhidi ya Caostal Union mjini Tanga, ikifuatiwa na Simba SC yenye pointi
23, ambayo leo imefungwa 2-0 na Mtibwa Sugar mjini Morogoro.
0 maoni:
Post a Comment