Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga (TRFA) uliochaguliwa katika
uchaguzi uliofanyika jana (Novemba 3 mwaka huu).
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TRFA walivyo na imani kubwa kwao katika
kusimamia mchezo huo mkoani Tanga.
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya TRFA ambayo imechaguliwa chini ya uenyekiti wa Said Soud.
Uongozi
huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha
shughuli za mpira wa miguu Tanga kwa kuzingatia katiba ya TRFA pamoja na
vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya TRFA na Kamati ya Uchaguzi ya
TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za
Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Viongozi
waliochaguliwa ni Said Soud (Mwenyekiti), Beatrice Mgaya (Katibu),
Khalid Mohamed (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF) na Juma Mgunda (Mwakilishi
wa Klabu TFF).
0 maoni:
Post a Comment