Kamisheni
ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) tayari imemtafutia bondia Francis
Cheka mpambano wa marudiano kati yake na bondia Chiotra Chimwemwe wa
Malawi katika jiji la Addis Ababa, Ehtiopia.
Mpambano
huo utafayika January 26, siku ya ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa nchi
za Africa (AU Summit) katika jiji hilo la Wafalme la Abesinia!
Cheka
na Chimwemwe watakutana jijini Arusha Desemba 26 (Boxing Day) katika
mpambano wa kutafuta nani mbabe wa uzito wa Super Middle katika bara la
Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG). Katika
mpambano huo mafahali hawa wawili wataumana kiume kwa raundi 12 za
dakika tatu kila mmoja!
Mpambano
wa Cheka na Chimwemwe jijini Arusha umeandaliwa na kampuni ya Screen
Hills (T) Investment ya jijini Dar-Es-Salaam inayomilikiwa na promota
maarufu aliyewahi kuwa bingwa wa taifa katika ngumi za ridhaa na kulipwa
Andrew George aka Chagga Boy!
Umaarufu
wa wawili hawa umewafanya mapromota wanaoandaa tamasha la kuchangisha
pesa kwa ajili ya kulisha watu wenye njaa katika bara la Africa
kuwaingiza Cheka 26(15)-6(3)-1 na Chiotra 26(15)-4(2)-1 katika mpambano hwa marudiano utakaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 26 Januaru 2012!
Katika
tamasha hilo, pambano kuu litakuwa kati ya bondia Oliver McCall
56(37)-12(1)-0 kutoka Marekani ambaye aliwahi kuwa bingwa wa uzito wa
juu duniani akipambana na bondia Sammy Retta - 18(17)-3(2)-0 kutoka
Ethiopia kugombea ubingwa wa IBF Africa, Mashariki ya Kati na Ghuba ya
Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa juu (Heavyweight)
Oliver McCall
Mapambano
mengine yatawakutanisha mabondia Daniel Wanyonyi 14(12)-5(2)-2 wa Kenya
atakayechuana na bondia Issac Hlatswayo 30(10)-5(3)-1 kutoka Afrika ya
Kusini katika kugombea ubingwa wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba
ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa Welterweight
Sammy Retta
Naye
Manzur Ali 7(4)-8(3)-0 bingwa wa uzito wa juu kutoka nchi ya Misri
atachuana vikali na bondia Harry Simon 27(20)-0-0 kutoka Namibia ubingwa
wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika
uzito wa Light heavyweight.
Mpambano
huu umeidhinishwa na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) na Cheka
kupewa kibali na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC).
0 maoni:
Post a Comment