Hoteli ya kitalii
Ikondolelo Lodge iliyoko Kibamba Jijini Dar es salaam , Imeteuliwa na Bodi ya
mashindano ya Miss Utalii Tanzania kuwa Hotel Rasmi ya mashindano hayo Mwaka
huu 2012.
Mchakato wa uteuzi ulihusisha Hotel zaidi ya saba zilizo
jitokeza kudhamini fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2012.
Kwa Ikondolelo kuwa
hotel Rasmi Miss utalii Tanzania itatumia zaidi ya Shilingi za kitanzania
Milioni mia moja , ikiwa ni udhamini wa gharama za kambi ya Warembo na
waandaaji zaidi ya sitini(60) kwa muda
wa wiki tatu.
Bodi katika kuteua
hotel rasmi ya mashindano mwaka huu imezingatia Vigezo vifuatavyo: Usalama wa
watu na mali zao, ubora wa viwango vya huduma ambayo siyo chini ya hadhi ya
nyota (3) , mazingira a hotel na utulivu wa eneo husika kulingana na viwango
vya kitaifa na Kimataifa vya mashindano ya Miss Utalii,pia kwa kuzingatia
viwango vilivyo wekwa na serikali kupitia Baraza la sanaa la Taifa (BASATA).
Warembo kutoka mikoa
yote ya Tanzania na Vyuo vikuu , wakiwa kambini katika Hotel ya Ikondolelo
watafanya shughuli mbalimbali za maandalizi na za kijamii; zikiwemo , Kujifunza
kuogelea katika bwawa lililopo hotelini hapo, Upigaji wa piga za minato katika
bustani zinazo zunguka hoteli, watapewa mafunzo maalum ya kutumia maeneo na
vifaa mbalimbali vya hotel za kitalii. Aidha washiriki wa fainali za taifa za
Miss utalii 2012 watapewa mafunzo kuhusiana na utalii, utamaduni, uwekezaji,
mazingira,afya ya jamii,elimu ya jamii uzalendo,watafundishwa mbinu za
kujieleza, kujiamini na kufanya matangazo.
Mkurugenzi mtendaji wa
Ikondolelo Lodge Ndugu Fredy Selekwa ameishukuru Bodi ya Miss utalii Tanzania
kwa kuwapa fulsa ya kuwa hotel Rasmi ya Mashindano haya muhimu kwa taifa katika
kukuza secta ya utalii na uchumi kwa ujumla. Ameihakikishia washiriki na viongozi
watakao kuwa kambini kuwapatia huduma zote muhimu kwa kiwango cha kimataifa
0 maoni:
Post a Comment