Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Idd
Mtiginjola kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF
iliyoundwa kutokana na marekebisho ya Katiba yaliyofanyika hivi
karibuni.
Mtiginjola
ambaye ni Wakili wa kujitegemea ataongoza kamati hiyo yenye wajumbe
watano ambayo sasa itakuwa chombo cha mwisho kusikiliza rufani
zinazotokana na uchaguzi wa TFF, na wanachama wa TFF ambao
hawatakubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Kabla
ya uteuzi huo, Mtiginjola alikuwa mjumbe wa Kamati ya Nidhamu ya TFF
inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana. Nafasi
yake katika kamati hiyo na ile ya mjumbe mwingine Kamishna Msaidizi wa
Polisi (ACP) Shabani Semlangwa aliyefariki dunia Julai mwaka huu
zitajazwa hivi karibuni.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF ambayo vinara wake
(Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti) wanatakiwa kitaaluma kuwa wanasheria
ni Francis Kabwe. Kabwe ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Wajumbe
wengine walioteuliwa na Kamati ya Utendaji ya TFF katika kikao chake
cha jana (Desemba 23 mwaka huu) ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama
Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP),
Mohamed Mpinga ambaye pia kitaaluma ni Mwanasheria.
Wengine
ni mshambuliaji wa zamani wa timu ya Reli Morogoro, Profesa Madundo
Mtambo ambaye kwa sasa ni Mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha
Sokoine (SUA) kilichopo mjini Morogoro, na mdau wa soka Murtaza Mangungu
ambaye pia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini.
0 maoni:
Post a Comment