Saturday, December 1, 2012

TIMU YA TAIFA YA TANZANIA BARA, THE KILIMANJARO STARS YATINGA ROBO FAINALI YAITANDIKA SOMALIA MABAO 7-0

Timu ya taifa ya TANZANIA BARA, THE KILIMANJARO STARS imetinga hatua ya robo fainali ya michuano ya 36 ya CECAFA baada ya kuifunga SOMALIA mabao SABA kwa BILA.
Winga Mshambuliaji wa Tanzania MRISHO NGASSA ndiye aliyekuwa mwiba mkali kwa walinzi wa SOMALIA baada ya kuvunja rekodi ya michuano hiyo kwa kufunga mabao MATANO na mabao MAWILI yakifungwa JOHN BOCCO.

Nayo timu ya ZANZIBAR imefungwa mabao mawili kwa bila dhidi ya MALAWI ,wakati timu ya RWANDA ikiibuka na ushindi wa mabao MAWILI kwa bila dhidi ya ERITREA na BURUNDI ikiifunga SUDAN bao moja kwa bila.

Kwa matokeo hayo timu zilizotoka katika mashindano hayo ni SOMALIA, ERITREA, SUDAN na SUDAN KUSINI.

Robo fainali ya michuano hiyo itaendelea jumatatu kwa timu ya KILIMAJARO STARS kucheza na RWANDA saa kumi jioni , UGANDA itacheza na ETHIOPIA wakati siku ya jumanne BURUNDI itacheza na ZANZIBAR na KENYA itacheza na MALAWI.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU