BONANZA la vyombo
mbalimbali vya habari lililopangwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu viwanja vya
Leaders Klabu likiandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA), sasa litafanyika viwanja vya Sigara (TCC), Chang’ombe pia Dar es
Salaam.
Uamuzi
wa kuhamisha bonanza hilo umechukuliwa na sekretarieti ya TASWA kutokana na
maombi ya waandishi wengi wa michezo kwa vile siku hiyo kuna mechi ya Kombe la
Shirikisho la Soka Afrika kati ya timu ya soka ya Azam na Barrack Young Controllers ya Liberia itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
siku hiyo.
Azam ni timu pekee ya Tanzania iliyobaki kwenye
michuano ya Afrika kwa ngazi ya klabu baada ya Simba na Jamhuri ya Pemba kutolewa
katika raundi ya awali.
Tunaamini kwa bonanza kufanyika Sigara itakuwa
rahisi kwa wadau wetu kushiriki kwenye bonanza na wale wengine watakaohitaji
kwenda uwanjani wafanye hivyo wakitokea Sigara kwa hakuna umbali mrefu na kisha
warejee kujumuika na wenzao mpaka mwisho.
Tunawaomba radhi
kwa mabadiliko hayo, lakini yakiwa na lengo la kujenga na kuwa pamoja na
wenzetu wa Azam kuhakikisha tunashirikiana nao kwa namna mbalimbali siku hiyo.
Bonanza hili
linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) likiwa na lengo la kuwaweka
pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya
na mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari ili
kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja.
Bonanza hilo
ambalo litahusisha wadau 1,500 kutoka vyombo mbalimbali vya habari litaambatana
na michezo mbalimbali itakayohusisha vyombo vyote vitakavyoshiriki na pia
kutakuwa na burudani ya muziki kutoka katika moja ya bendi kubwa za muziki wa
dansi hapa nchini, ambayo itatangazwa siku zijazo.
0 maoni:
Post a Comment