Mshindi
wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award kutoka Mkoa wa Arusha
Rose Godwin, Akiwa anasogea Mbele Mara Baada ya Kutangazwa kuwa ndiye
mshindi wa Tuzo hiyo.
Mshindi
wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award kutoka Mkoa wa Arusha
Rose Godwin akivalishwa Skafu maalum ya ushindi na Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye
Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award kutoka Mkoa wa Arusha Rose Godwin akikabidhiwa ua na Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya chuo cha uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma Drk. Herbert Makoye
Mshindi
wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award nafasi ya Tatu Baby
Juma kutoka mkoa wa Mtwara Akikabidhiwa Zawadi ya Ua na Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye
Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award nafasi ya pili kutoka Mkoa wa Rukwa Neema Kafanunzi Akikabidhiwa Zawadi ya Ua na Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye
Mshindi
wa Tuzo ya Media ya Awards kutoka mkoa wa Arusha(katikati) akiwa na
wenzake baada ya kutangazwa mrembo wa Vyombo vya Habari vya SJMC Radio,
Tv na Magazeti, hafla ambayo imefanyika kwenye ofisi za Chuo Kijitonyama
jijini Dar es salaam. Fainali za Miss Utalii zitafanyika tarhe
6/4/2012/13 katika Viwanja vya Makumbusho.
Mwalimu
Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert
Makoye (wa pili kulia), akiwa na Washindi wa watatu wa Tuzo ya Media
Awards ya chuo hicho, katikati ni mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo kutoka
katika Mkoa wa Arusha.
Rais wa Miss Utalii Tanzania wa Kwanza kutoka upande wa kushoto Ndugu Erasto G. Chipungahelo Akiwa Na washindi watatu pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye.
Meneja
vyombo vya habari vya Mlimani-Mama Edda Sanga(kati) Susanne
Mbise(kushoto)na Afisa Masoko wa SJMC Sophia Ndibalema(kulia) wakiwa na
Mshindi wa Miss Utalii Tanzania-Tuzo ya Media Awards kutoka mkoa wa
Arusha, muda Mfupi baada ya kutangazwa katika Hafla iliyofanyika katika
Chuo cha SJMC.
Washiriki
wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakiwa katika picha ya pamoja Mara
baada ya kutangazwa kwa Mshindi wa tuzo ya SJMC Media Award
Jopo la majaji wakiwa katika Picha ya Pamoja
Rais wa Miss Utalii Tanzania Ndugu Erasto G. Chipungahelo akitoa neno la Shukurani kwa Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye ofisini kwake
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakitumbuiza Ngoma za asili wakati wa utoaji wa Tuzo hiyo.
Washindi sita wakiwa katika Picha ya Pamoja
Fainali
za Utalii Tanzania zimeendelea kushika kasi kwa warembo kushindania
Tuzo mbalimbali za Utalii, Utamaduni, Jamii na za Kuichumi. Jana
lilifanyika Shindano la kumpata Mshindi wa Tuzo ya Habari (Media
Award) , Shindano ambalo liloifanyika katika Viunga vya Chuo Kikuu cha
Dar es salaam , Shule kuu ya uandishi wa Habari na Mawasiliano ya umma
(SJMC) ambao ni wadhamini wakuu wa Tuzo hiyo.
Katika
Shindano hilo la Miss Utalii Tanzania 2012/13 Media Award zaidi ya
Warembo 30 walipanda jukwaani kwa kuelezea mada ya vivutio vya Mikoa
wanayo wakirisha na kisha Majaji wa Shindano hilo kutoka Shule Kuu ya
Waandishi wa Habari na mawasiliano ya Umma walitangaza warembo Sita
walioingia katika Sita Bora na Baadae waliulizwa Maswali kila mmoja na
swali lake na pia swali la pili lilikuwa ni Swali la Jumla ambapo wote
waliulizwa. Washiriki wote walijibu kwa umahili na baadae wakapatikana
washindi watatu ambapo Mshindi wa kwanza alikuwa ni Miss Utalii Tanzania
2012/13 kutoka Mkoa wa Arusha Rose Godwin, Mshindi wa Pili alikuwa Miss
Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Rukwa Neema Kafanunzi na Mshindi
wa tatu alikuwa Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Mtwara Baby
Juma.
Mshindi wa Tuzo hiyo ya Mshindi
wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award kutoka Mkoa wa
Arusha Rose Godwin Alipata zawadi ya Udhamini wa kusomeshwa katika
Shule Kuu hiyo ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Mara baada ya kutoa Tuzo, Rais wa Miss Utalii
Tanzania Aliwashukuru Wadhamini wakuu wa Tuzo hiyo ya SJMC Miss Tourism
Tanzania 2012/13 Media Awards, ambao ni Shule Kuu ya Uandishi wa Habari
na Mawasiliano ya Umma kwa kutoa Heshima kubwa ya Kumsomesha Mshindi wa
Tuzo hiyo katika chuo hicho na kuongeza kuwa Elimu ndio Ufunguo wa
Maisha na Hilo ni Jambo muhimu katika Taifa letu la Tanzania ambapo
Wasomi zaidi wanahitajika ili Kujenga Taifa na Kukuza Uchumi wa nchi
yetu.
0 maoni:
Post a Comment