Bondia Jeffrey Mathebula akigawa dozi
Mabondia wa
Afrika ya Kusini Jeffrey Mathebula na Takalani Ndlovu watakutana katika ukumbi wa Carnival City Casino jijini Johannesburg
jimbo la Gauteng nchini Afrika ya Kusini katika pambano la mchujo (Elimination
Title) la ubingwa wa dunia uzito wa unyoya (Featherweight).
Wawili hawa ni mahasimu
wakubwa wanaojulikana nchini Afrika ya Kusini na walishakutana mara
mbili ambapo Ndlovu alishhinda pambano la awali huku Mathebula akishinda
pambano la mwisho.
Wakati huo huo mabondia Vusi Malinga wa Afrika ya Kusini na Diarh Gabutan wa
Phillipines watakutana katika mpambano mwingine wa mchujo kuwania tiketi ya
kukutana na bingwa wa dunia katika uzito wa Bantam.
Promota maarufu wa Afrika ya Kusini Branco Milenkovic wa kampuni ya
Branco Boxing Promitions atakuwa ndiye mwandaaji wa mpambano huo utakaofanyika
tarehe 23 mwezi wa tatu mwaka huu.
Huu ni mwendelezo wa Shirikisho la Ngumi la kKmataifa IBF katika
programu yake ua “Utalii wa Michezo” barani Afrika ambapo imejiwekea lengo la
mapambano 100 ya ubingwa mwaka huu.
0 maoni:
Post a Comment