Friday, March 15, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAJI YA DAWASA RUVU CHINI MKOA WA PWANI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi Mji mpya wa Mabwe Pande (hawapo pichani) wakati alipofika katika mji huo jana Machi 14, 2013 akiwa katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya Maji inayosimamiwa na Dawasa na kutembelea katika Mtambo wa Ruvu Chini kukagua kazi zinazoendelea za upanuzi wa Mtambo huo wa Ruvu chini. Kulia ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Saidik.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa miradi ya Maji, William Kazenga, kuhusu upanuzi wa mtambo wa Ruvu chini wa kusambaza maji, wakati Makamu alipofika eneo hilo jana Machi 14, 2013 kwa ajili ya kukagua kazi zinazoendelea za upanuzi wa Mtambo huo wa Ruvu chini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa miradi ya Maji, William Kazenga, kuhusu upanuzi wa mtambo wa Ruvu chini wa kusambaza maji, wakati Makamu alipofika eneo hilo jana Machi 14, 2013 kwa ajili ya kukagua kazi zinazoendelea za upanuzi wa Mtambo huo wa Ruvu chini. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi (wa pili kushoto) ni Waziri wa Maji na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea kukagua kazi zinazoendelea za upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu chini jana Machi 14, 2013 wakati Makamu alipofika eneo hilo jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, Waziri wa Maji, Jumanne Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantum Mahiza na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na viongozi wa Dawasa baada ya Makamu kutembelea na kukagua kazi zinazoendelea za upanuzi wa Mtambo wa Ruvu chini, jana Machi 14, 2013. Picha na OMR.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU