Meneja Bidhaa wa Coca-Cola Tanzania Bw. Maurice Njowoka
akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo
kwa ajili ya mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 15 ya Copa Coca-cola
ngazi ya wilaya. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
Afisa Maendeleo ya soka wa TFF Bw. Salum Madadi akiongea na
waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukubidhiwa vifaa vya michezo kwa ajili
ya mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 15 ya Copa Coca-cola ngazi ya
wilaya. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki..
Meneja Bidhaa wa
Coca-Cola Tanzania Bw. Maurice Njowoka (kulia) akimkabidhi Afisa Maendeleo ya
soka wa TFF Bw. Salum Madadi vifaa vya michezo kwa ajili ya Copa Coca-Cola
ngazi ya wilaya. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
Coca-Cola imelikabidhi Shirikisho
la Mprira wa Miguu nchini (TFF) mipira na bibs kwa ajili ya timu zinazoshiriki
mashindano ya soka ya vijana ya Copa Coca-Cola ambayo kuanzia mwaka huu yatakuwa
ya umri chini ya miaka 15 badala ya chini ya miaka 17 kama ilivyokuwa miaka
iliyopita.
Lengo la kubadili umri kama
ilivyoshauriwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ni kuweza
kuwafikia vijana wadogo zaidi na hivyo kuwa na wigo mpana wa kukuza vipaji vyao
kwa muda mrefu zaidi kabla hawajachukuliwa na vilabu vikubwa.
Vifaa vilivyotolewa na Coca-Cola na
kupokelewa na Afisa Maendeleo ya soka wa TFF Bw Salum Madadi vitatumika ngazi
ya wilaya. Akipokea vifaa hivyo, Bw. Madadi amewataka viongozi wa soka ngazi ya
wilaya na mikoa kuzingatia kanuni na taratibu za Copa Coca-Cola. Hafla ya
kukabidhi vifaa hivyo ilifanyika ofisi za Coca-Cola Tanzania jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Alisema kuwa baadhi ya wilaya
tayari zimeshaanza mechi za michuano hiyo ya vijana na kuzitaka wilaya ambazo
zilikuwa zinasubiri vifaa ili kuanza kucheza kufanya hivyo mara moja kwa kuwa
sasa vifaa viko tayari.
Akizungumza kabla ya kukabidhi
vifaa hivyo, Meneja Bidhaa wa Coca-Cola Tanzania Maurice Njowoka alisistiza msimamo thabithi wa
Coca-Cola wa kuendelea kudhamini mashindano ya Copa Coca-Cola ambayo yamekuwa
chimbuko la wanasoka chipukizi nchini Tanzania.
“Tumeamua kubadili mashindano ya
Copa Coca-Cola kuwa ya umri chini ya miaka 15 badala ya chini ya umiri wa miaka
17 kama ilivyokuwa miaka iliyopita ili kutoa fursa kwa vijana wadogo zaidi
kufundishwa na kuendeleza vipaji vyao na kupata uzoefu mapema zaidi,” alisema Njowoka.
Barani Africa, mashindano ya soka ya vijana
ya Copa Coca-Cola hufanyika katika nchi zaidi ya 20 na kushirikisha zaidi ya
wachezaji chipukizi zaidi ya 50,000. Miaka iliyopita Copa Coca-cola imeweza
kuibua vipaji vya wachezaji nyota ikiwa ni pamoja na mlinda mlango wa timu ya
Taifa ya Zambia Kennedy Mweene na wachezaji wenginie Nathan Sinkala na tophila
Sunzu; Uganda ni pamoja na mlinzi wa kimataifa Timothy Batabaire; Nigeria ni
kiungo wa FC Porto Mikel Agu; Kenya ni kiungo mahili Donald Mariga; Tanzania ni
mshambuliaji Thomas Ulimwengu; na Afrika Kusini Mandla Masango na Happy Jele.
Hawa ni kwa uchache tu.
“Tuna nyota wengi wanaoibuka kutokana na
mashindano ya Copa Coca-Cola kila mwaka,” anasema Njowoka. “Wachezaji
waliofanikiwa wamekuwa ni chachu ya sisi kujisikia fahari na kuendelea
kudhamini mashindano hayo. Wachezaji wanaojituma na kufanikiwa ni mashujaa.
Wazazi wanaowapa moyo vijana wao na kuwaongoza ni mashujaa. Makocha wanaojitoa
kwa moyo mmoja kufundisha vijana ni mashujaa. Hata washabiki wanaojitokeza
kuwatia moyo wachezaji pia ni mashujaa. Hii inakuwenda sanjali na kauli mbiu
yetu kwamba Copa Coca-cola ni mashindano yanazaa mashujaa,” alisema.
Mashindano ya mwaka huu yanafuatia ya mwaka jana yaliyofana
katika nchi zaidi ya 20 barani Afrika ambapo vijana 134 walipata fursa ya
kwenda Afrika Kusini kushiriki kambi ya mafunzo ya soka kwa wiki mbili





0 maoni:
Post a Comment