Muuguzi
wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road
(ORCI) Sr. Felista John (katikati
aliyevaa gauni jeupe) akipokea msaada wa vyakula mbalimbali kutoka Meneja Uendeshaji Mikopo wa Benki ya
Taifa ya Biashara (NBC), Mwanaisha Ayosi, iliyotolewa na benki hiyo kitengo cha
Operesheni ikiwa ni moja ya mikakati ya benki hiyo kusaidia shughuli za kijamii
hospitalini hapo. Wengine ni wafanyakazi katika kitengo hicho.
moja wa wafanyakazi wa maofisa wa benki ya NBC, Lioba
Massao (kushoto) akifanya maombezi kwa baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika
wodi ya Taasisi ya Saratani ya Ocean
Road (ORCI) katika hafla ambayo benki
hiyo kitengo cha operesheni kilikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali ikiwa ni moja ya
mikakati ya benki hiyo kusaidia shughuli za kijamii hospitalini hapo
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakimjulia hali mmoja wa
wagonjwa waliolazwa katika taasisi hiyo mara baada ya kukabidhi msaada wa aina
mbalimbali za vyakula.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakimjulia hali mmoja wa
wagonjwa waliolazwa katika taasisi hiyo na pia kumkabidhi msaada wa sabuni ya
kufulia.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakibeba mizigo ya vyakula
na mafuta ya kupikia tayari kuwakabidhi wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya
Saratani ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam kama sehemu ya juhudi za NBC
katika kusaidia shughuli za jamii.





0 maoni:
Post a Comment