Tuesday, May 28, 2013

TANZANIA YAJIANDAA KWA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA CHESS!

 https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=c5efcfe0c1&view=att&th=13eeb70f9233e5b4&attid=0.3&disp=inline&realattid=f_hh95k5jl2&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-2CrkZwFZoIv7yIISqZzQc&sadet=1369753310560&sads=naENlw7uPP6cgOI9fxWTxGiJ07Q
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=c5efcfe0c1&view=att&th=13eeb7d738f0825c&attid=0.1&disp=inline&realattid=f_hh95uyyt0&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-2CrkZwFZoIv7yIISqZzQc&sadet=1369754421390&sads=iScoAxsifNbsLhsKex5b8h1DxYc 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Spicenet Tanzania Ltd, Vinay Choudary (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mashindano ya Kimataifa ya mchezo wa Chess yatakayoanza Juni 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Michezo katika Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Benson Chacha, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Chess Tanzania, Joe Anea na mjumbe wa kamati ya chama cha chess, Emmanuel Mwaisumbe.
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=c5efcfe0c1&view=att&th=13eeb7d738f0825c&attid=0.2&disp=inline&realattid=f_hh95v2671&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-2CrkZwFZoIv7yIISqZzQc&sadet=1369754431153&sads=IqguMrf5RUSS5UyD7ARPm8TXVr8 
Raisi wa Chama cha Chess Tanzania (TACA), Geoffrey Mwanyika (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mashindano ya Kimataifa ya mchezo wa Chess yatakayoanza Juni 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Michezo katika Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Benson Chacha, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Chess Tanzania, Joe Anea na mjumbe wa kamati ya chama cha chess, Emmanuel Mwaisumbe.
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=c5efcfe0c1&view=att&th=13eeb7d738f0825c&attid=0.3&disp=inline&realattid=f_hh95v4l12&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-2CrkZwFZoIv7yIISqZzQc&sadet=1369754427443&sads=R7BuhqDcyMag8CEpazSy9fZ0m-8 
Baadhi ya wapiga picha za habari wakirekodi tukio hilo jijini Dar es Salaam leo.
 
Katika jitihada za kuufufua mchezo wa Chess nchini, Chama cha Chess Tanzania kwa kushirikiana na Spicenet Tanzania Limited moja ya makampuni yanayoongoza kwa kutoa huduma za intaneti hapa nchini, wameandaa mashindano ya wazi ya kimataifa yajulikanayo kama Spicenet Tanzania Open Chess Championship 2013 ambayo yatahusisha wachezaji kutoka Tanzania, Zambia, Uganda, Kenya, Msumbiji na Uingereza.


Mashindano hayo ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 14 hadi 16 Juni 2013, katika ukumbi wa Meru uliopo katika jingo la Golden Jubilee Tower Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam, ni ya kiwango cha FIDE (Shirikisho la Chess Duniani) na ni moja ya mashindano magumu kabisa yaliyowahi kuchezwa ndani ya muongo mmoja katika Afrika Mashariki.

Katika kunogesha, Bingwa – GM Nigel Short, ambaye alikuwa ni mchezaji namba 3 duniani mwaka 1990 na mpinzani wa Garry Kasparov, mchezaji mdogo kabisa na bingwa wa zamani wa Chess Duniani ambaye anachukuliwa kama mchezaji bora kabisa wa wakati wote, atakuwa mmoja wa washiriki.


Mashindano haya yanaweka rekodi Afrika Mashariki kwa kuwa la kwanza katika historia ya Chess katika ukanda huu kumualika Bingwa huyo. Pamoja na Nigel mwenye cheo cha Grandmaster,  mabigwa watatu wenye cheo cha International Master watashiriki kutoka Zambia na wengine wenye cheo cha Fide Master kutoka Uganda. Jumla ya washiriki inatazamiwa kuwa 80, huku wachezaji 50 wakitoka Tanzania na 30 kutoka nchi za jirani.

Akizungumzia udhamini wao kwenye mchezo huo, Mkurugenzi wa Spicenet, Vinay Choudary alisema wameamua kuunganisha nguvu na Chama cha Chess Tanzania kuufufua mchezo huo Tanzania katika jitihada za kuhakikisha kwamba nchi yetu inang’ara katika medani ya michezo katika mashindano ya kimataifa.


“Tumeamua kudhamini mchezo huu kwa sababu tunaamini kwamba tuna wachezaji wazuri ambao wanaweza kufikia viwango vya kimataifa na kuiletea nchi yetu sifa katika michezo” alisema Vinay akiongeza kwamba nia yetu ni kukisaidia Chama cha Chess kuhakikisha mchezo huo unatangazwa na hatimaye kutambulishwa kwa watu wengi kupitia shule, taasisi, vyuo vikuu na njia nyinginezo. Hii itatuhakikishia kuwa na timu nzuri ya taifa ambayo inaweza kushiriki na kushinda katika mashindano ya kimataifa.


Kwa upande wake,  makamu Mwenyekiti wa Chama cha Chess Tanzania, Joe Anea alisema wanajivunia udhamini uliotolewa na Spicenet kwa mchezo huo na alielezea kuwa msaada kama huo ni muhimu katika kuufufua na kuutangaza mchezo huo nchini.

Kuhusiana na zawadi, Mwenyekiti alisema kutakuwa na jumla ya washindi watano ambapo mshindi wa nafasi ya kwanza atapokea shilingi za Kitanzania 1,000,000; nafasi ya pili shilingi 500,000; nafasi ya tatu shilingi 300,000 na nafasi za nne na tano shilingi 100,000 kila mmoja.


Afisa wa Baraza la Michezo la Taifa BMT Benson Chacha, amesema wakati umefika kwa watu kuweka nguvu zaidi katika michezo mingine mbali na ile iliyozoeleka ili kuongeza wigo wa taifa kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa. “ni muhimu wadau wakaangalia uwezekano wa kuiimarisha michezo midogomidogo kwani ina fursa kubwa sana ya kututangaza kimataifa” alisema Benson na kusisitiza kuwa BMT itaendelea kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa wadau wa michezo yote bila kubagua ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inakuwa na michezo mingi zaidi kwa manufaa ya wachezaji na jamii kwa ujumla.


Chess ni mchezo wa mkakati wa watu wawili unaochezwa kwenye Ubao wa Chess wenye miraba 64 iliyopangwa katika mfumo wa nane kwa nane. Ni mchezo unaotambulika na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki na kusimamiwa na Shirikisho la Dunia la Chess (FIDE) ambalo linaandaa mashindano ya Chess Olympiad  kila baada ya miaka miwili.

Katika Tanzania mchezo wa chess ulikuwa unasimamiwa na Chama cha Chess Tanzania ambacho kilianzishwa na kusajiliwa chini ya Baraza la Michezo la Taifa mwaka 1984, na mpaka mwaka 1998 mchezo ulikuwa ukichezwa sana. Baada ya hapo ulipotea na hivyo mwaka 2010 ulianzishwa tena na mwaka 2012 Kamati ya Muda iliundwa kuendesha Chama cha Chess Tanzania.


0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU