
KLABU ya SIMBA imekamilisha
usajili wa wachezaji wake ambao benchi la ufundi la klabu hiyo iliwataka na
hivyo kubaki na mchezaji mmoja wa kigeni ambaye kwa sasa wanamalizia mipango ya
usajili katika klabu ya SIMBA.
MWENYEKITI wa kamati ya
usajili wa Klabu hiyo, ZAKARIA HANSPOP amesema klabu yake inaimani kuwa wachezaji
iliyowasajili wataisaidia Simba katika michezo yake.
SIMBA imeshasajili wachezaji
ISSA RASHID maarufu kama baba ubaya kutoka MTIBWA SUGAR, ZAHORO PAZI kutoka wa
AZAM FC ambaye alikuwa akicheza kwa mkopo katika klabu ya JKT RUVU, ANDREW
NTALLA wa KAGERA SUGAR,TWAHA SHEKUWE MESSI kutoka COASTAL UNION ya TANGA na
SAMUEL SSENKOOMI kutoa URA ya UGANDA.
Ratiba ya klabu ya SIMBA kwa
sasa ni kusubiri matayarisho ya kujiandaa na mashindano ya vilabu ya Afrika
mashariki na kati ya KAGAME yaliyopangwa kufanyika katika mji wa JUBA uliopo SUDAN KUSINI.





0 maoni:
Post a Comment