Meya wa Manispaa ya Tabora
katikati Akimkabidhi kiongozi wa kundi la Mwenge fedha tasilimu
shilingi laki sita mara baada ya kundi hilo kutangazwa Washindi wa shindano
la ngoma za asili kwa mkoa wa Tabora ambalo limefadhiriwa na kampuni ya
Bia Tanzania Tbl kupitia Bia yake ya Balimi Extra kulia kwake ni Meneja
matukio wa kampuni hiyo kanda ya Ziwa Bw Eric Mwayela.
Kushoto meneja wa matukio wa kampuni ya Bia Tanzania - tbl kanda ya ziwa
Bwana Erick Mwayela akimkabidhi Meya wa Manispaa ya Tabora Mstahiki
Meya Gulamhussein Remtullah kitita cha shilingi laki sita ikiwa ni
zawadi ya mshindi wa kwanza wa mashindano ya Ngoma za asili kwa mkoa wa
Tabora mashindano hayo yamedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania kupitia
Bia yake ya Balimi Extra kulia aliyevaa fulani ya balimi ni kiongozi wa
kundi la Mwenge la manispaa hiyo ambao ndio wameibuka washindi wa
shindano hilo.
Mgeni rasmi katika mashindano ya ngoma za asili kwa Mkoa wa Tabora
Mstahiki Meya wa manispaa ya Tabora Gulamhussein Remtullah akizungumza
na wakazi wa Mkoa huo katika mashindano hayo chini ya udhamini wa
kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya Balimi Extra , mashindano
hayo yamefanyika katika shule ya sekondari Iyungi.tolle.
Hatimaye fainali za mashindano ya
ngoma za asili kwa mkoa wa tabora ambayo yamedhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania-TBL
kupitia bia yake ya balimi extra yamemalizika rasmi kwa kundi la mwenge kuibuka
bingwa wa mashindano hayo na kujinyakulia kitita cha shilingi laki 6 na hivyo
kupata tiketi ya kuuwakilisha mkoa huo katika mashindano ya kanda yatakayo
fanyika jijini mwanza hivi karibuni.
Katika kinyang'anyilo hicho ambacho
kimevuta hisia za wakazi wengi wa mkoa huo, kundi hilo limeibuka mshindi kwa
alama 90 likifuatiwa na kundi la magereza ambayo imepata alama 87 na kuondoka
na zawadi ya shilingi laki 5 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na masange jkt
ambao wamejinyakulia shilingi laki 400 kwa kupata alama 77, nafasi ya 4
imechukuliwa na kundi la mwamko sikonge na kujipatia shilingi laki 3kwa kupata
alama 63.
Katika mpambano huo ambao
umevishirikisha vikundi 10 washiriki wote kuanzia nafasi ya 5 mpaka ya 10
wamejinyakulia zawadi ya fedha tasilimu shilingi laki moja na nusu huku meya wa
manispaa hiyo mstahiki meya gulamhussein remtullah ambaye ndiye aliye kuwa
mgeni rasmi akiipongeza kampuni hiyo kwa kudhamini mashindano hayo ambapo
kupitia mashindano hayo jamii imekuwa ikijikumbusha tamaduni zetu.
Gulamhussein amesema kutokana na
kampuni hiyo kufanya mashindano hayo katika kipindi hiki cha mavuno hii
inadhirisha kwamba bia hiyo ya balimi extra inamjali na kumsamini mkulima wa
kitanzania.
Aidha meya huyo amelitaka kundu hilo
la mwenge kwenda kuuwakilisha vyema mkoa wa tabora na kuhakikisha kuwa
wanalejea na ushindi katika mashindano ya kanda ambayo yanatalajia kufanyika
jijini mwanza hivi karibuni.
Awali meneja wa matukio wa kanda ya
ziwa bwana erick mwayela amesema kuwa kampuni yake kupitia bia ya balimi extra
wanajisikia fahari kudhamini mashindano hayo ambapo amefafanua kuwa kupitia
mashindano hayo watu wamekuwa wakifahamiana na kukumbuka ngoma za asili za
makabila yetu.
Mashindano mengine kama hayo
yanatalajiwa kufanyika mjini shinyanga mwishoni mwa wiki ijayo ambapo vikundi
mbalimbali vya mkoa huwa vitapata fulsa ya kushiriki katika mpambano huo na
hivyo kuwataka wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia mwakilishi
wao katika mashindano ya kanda.
0 maoni:
Post a Comment