Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa
picha ya X-Ray, ya mmoja kati ya majeruhi waliolazwa
kwenye Hospitali ya Mount Meru, Joseph Anthony, mkazi wa Karoleni,
baada ya kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu lililotokea wiki iliyopita
katika mkutano wa Chadema eneo la Soweto jijini Arusha. Imeelezwa kuwa
hadi jana Juni 17, 2013, wakati makamu alipowatembelea majeruhi hao watu watatu waliliripotiwa kufariki dunia.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza
na wananchi wa jijini Arusha waliokusanyika nje
ya Hospitali ya Mount Meru jana, wakati Makamu alipokuwa na ziara ya
kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko wa Bomu uliotokea wiki
iliyopita katika mkutano wa Chadema jijini Arusha, ambapo jumla ya watu
70 walijeruhiwa na watatu walifariki dunia. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mwilongo.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia
hali Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari,
aliyelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Selian, mkoani Arusha baada ya
kudaiwa kushambuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akiwa
katika uchaguzi mdogo wa Udiwani wa Kata ya Makuyuni, Monduli. Awali
Nasari alikaririwa akieleza kuwa anamaumivu ya mgongo baada ya kushambuliwa
na vitu vigumu na vijana wa Kimasai. Kwa mujibu wa maelezo ya Mganga
Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Paul Kweka, anayemtibu Mbunge huyo, alimueleza Makamu wa Rais kuwa mbunge huyo, baada
ya kupimwa na kupigwa picha za X-Ray, ameonekana kuwa hana tatizo lolote
la kiafya.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza
maelezo kutoka kwa Dkt. Geofrey, kuhusu jinsi
mtoto, Aboubakar Adam, mkazi wa Sakina jijini Arusha, aliyelazwa katika
Hospitali ya ARumeru baada ya kujeruhiwa na bomu wakati akiwa
miongoni mwa watu waliokuwa katika Uwanja wa Soweto kwenye Mkutano wa
Chadema wiki iliyopita. Makamu wa Rais, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa
mlipuko huo, waliolazwa katika Hospitali za Arumeru, Selian na Mtakatifu
Elizabeth, jana Juni 17, 2013
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali, Gabriel Kivuyo (52) aliyelazwa Hospitali
ya Rufaa Selian, baada ya kujeruhiwa na mlipuko wa bomu katika mkutano
wa Chadema, mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha. Makamu
wa Rais, jana Juni 17, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali
majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa katika hospitali za Mount Meru, Selian na Mtakatifu Elizabeth.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia
hali, mtoto aliyetambuliwa kwa jina moja la Fahad
(7) aliyelazwa katika chumba cha watu mahututi Hospitali ya Rufaa
Selian, baada ya kujeruhiwa na mlipuko wa bomu katika mkutano wa Chadema,
mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha. Makamu wa Rais, jana Juni
17, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa katika hospitali za Mount Meru, Selian na Mtakatifu
Elizabeth.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia
hali, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Majengo
A, Sarah John (45) aliyelazwa Hospitali ya Mtakatifu Elizabeth, baada
ya kujeruhiwa na mlipuko wa bomu katika mkutano wa Chadema, mwishoni
mwa wiki iliyopita jijini Arusha. Makamu wa Rais, jana Juni 17,
alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa katika hospitali za Mount Meru, Selian na Mtakatifu Elizabeth. Picha na OMR
0 maoni:
Post a Comment