Tuesday, June 25, 2013

PAMABANO LA VUNJA JUNGU

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=c5efcfe0c1&view=att&th=13f7a3129429ffb8&attid=0.3&disp=inline&realattid=f_hico9cu92&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-2CrkZwFZoIv7yIISqZzQc&sadet=1372166012117&sads=5047SRowuzobXMZE5INH2NXJfCU 
 Yohana Uso Kwa Uso Mabondia Wakali Ulingo na Watakatifu Nje ya Ulingo. Yohana Robert na Yohana Mathayo
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=c5efcfe0c1&view=att&th=13f7a3129429ffb8&attid=0.4&disp=inline&realattid=f_hicoa7l03&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-2CrkZwFZoIv7yIISqZzQc&sadet=1372166018277&sads=zhNRD2CpmjdLhogZZTN0IS4awLI
Mabondia Yohana Mathayo na Yohana Robert Wakitunishiana Misuli


kuna pambano la ngumi la aina yake katika historia ya ngumi ambalo litapigwa siku tarehe 30/6/2013 ambayo ni wiki ya mwisho kabla ya kuingia mwezi wa ramadhan,ambapo waumini wa dini ya kiislam hufunga na shughuli nyingi za starehe ,michezo na anasa nyingine hupungua ndani ya mwezi huo, hivyo ni wiki la vunja jungu ndio pambano la mabondia wakatili ulingoni na wapole nje ya ulingo na wacha mungu sana YOHANA ROBERT NA YOHANA MATHAYO watazipiga katika ukumbi wa friends corner hotel pale manzese. ni pambano lenye upinzani mkali kutokana na sifa za mabondia wenyewe kutokuwa na mzaha wawapo ulingoni na ni mabondia wasiokubali kushindwa, hiyo nayo ni sifa mojawapo inayowafanya wawe na rekodi nzuri katika ngumi za kulipwa hapa nchini.
 
akilizungumzia pambano hilo Ibrahim kamwe kwa niaba ya muandaaji mkuu mwalim hatibu anasema kuwa maandalizi yamekwenda vizuri na mpaka sasa hakuna tatizo lolote kwa mabondia hao watakaocheza pambano kuu wala wale wa utangulizi ambao ni   Fabian lyimo  atazipiga na musa sunga pambano la raund nane huku Bakari ustadh atazipiga na frank zagarino, wakati huohuo Tasha mjuaji na Rama johncena watatoana jasho. Pia Yule bingwa wa PST uzito mdogo (minimum weight) goldsilver ataumana vikali na bondia kutoka klabu ya bigright boxing herman Richard. Nae Ibrahim kamwe anaongeza kwa kusema hilo, linaweza kuwa pambano kali sana la vunja jungu ambalo halijawahi kutokea kutokana na sifa na mabondia wenyewe na jinsi walivyo kamiana na uwezo mzuri wa kutupa makonde walionao  

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU