Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Coastal Union iliyochezwa
jana (Agosti 28 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
imeingiza sh. 152,296,000.
Watazamaji 26,137 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 14 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Viingilio
katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 36,947,427.45 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 23,231,593.22.
Mgawo
mwingine ni asilimia 15 ya uwanja sh. 18,786,827.52, tiketi sh.
3,818,890, gharama za mechi sh. 11,272,096.51, Kamati ya Ligi sh.
11,272,096.51, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
5,636,048.26 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 4,383,593.09.
COPA COCA-COLA KANDA KUANZA SEPT 2
Michuano
ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15
inayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani inaanza kutimua
vumbi Septemba 2 mwaka huu katika vituo sita tofauti.
Kwa
mujibu wa ratiba iliyopangwa leo (Agosti 29 mwaka huu), kituo cha
Mwanza mechi zake zitachezwa katika viwanja vya Alliance ambapo timu
zitakazofungua dimba ni Kagera vs Kigoma, Mara vs Tabora, Simiyu vs
Geita na Mwanza vs Shinyanga.
Kituo
cha Mbeya ambapo mechi zitachezwa viwanja vya Iyunga ni Katavi vs
Njombe, na Ruvuma vs Mbeya. Kituo cha Pwani ni Ilala vs Kaskazini
Unguja, na Lindi vs Pwani.
Ufunguzi
katika kituo cha Arusha ambapo mechi zake zitachezwa Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta AMri Abeid ni Manyara vs Kilimanjaro, na
Arusha vs Singida.
Uwanja
wa Jamhuri ambapo utatumika kwa mechi za kituo cha Morogoro, Tanga
itacheza na Dodoma wakati Morogoro itaumana na Temeke. Mjini Zanibar
kwenye Uwanja wa Chuo cha Amaan ni kati ya Kaskazini Pemba na Mjini
Magharibi, na Kusini Pemba dhidi ya Kusini Unguja.
USAILI WAGOMBEA TFF, TPL BOARD KUANZA KESHO
Usaili
kwa wanaoomba kuteuliwa kuwa wagombea uongozi katika uchaguzi wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na ule wa Bodi wa Ligi Kuu
(TPL Board) unaanza kesho (Agosti 30 mwaka huu).
Kwa
mujibu wa ratiba iliyotolewa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Agosti 30
mwaka huu ni usaili kwa waombaji uongozi wote katika Bodi ya Ligi Kuu
pamoja na waombaji uongozi wa TFF kwa kanda namba 11 (Morogoro na
Pwani), kanda namba 12 (Kilimanjaro na Tanga) na kanda namba 13 (Dar es
Salaam).
Agosti
31 mwaka huu ni kanda namba sita (Rukwa na Katavi), kanda namba saba
(Mbeya na Iringa), kanda namba nane (Njombe na Ruvuma), kanda namba tisa
(Lindi na Mtwara) na kanda namba kumi (Dodoma na Singida).
Usaili
kwa kanda namba moja (Geita na Kagera), kanda namba mbili (Mara na
Mwanza), kanda namba tatu (Simiyu na Shinyanga), kanda namba nne (Arusha
na Manyara) kanda namba tano (Kigoma na Tabora), na nafasi za Rais na
Makamu wa Rais wa TFF utafanyika Septemba Mosi mwaka huu.
Waombaji
wote wamepangiwa muda wao wa usaili. Kwa mujibu wa ratiba usaili
ufanyika kuanzia saa 3 kamili asubuhi hadi saa 2 usiku. Wasailiwa wote
wanatakiwa kuzingatia muda waliopangiwa.
0 maoni:
Post a Comment