Monday, August 26, 2013

MPO AFRIKA YATWAA UBINGWA SAFARI POOL TEMEKE

 Baadhi ya wachezaji wa Klabu ya Mpo Afrika wakishangilia na Kikombe mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa,Mkoa wa Temeke iliyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mpo Afrika ilishinda 13-11 dhidi ya Klabu ya Sun City

 Katibu Mkuu wa chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos Kafwinga akimkabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi 350,000/= bingwa wa mchezaji mmoja mmoja wanaume(Singles), Sulemani Cato mara baada ya kumfunga Nahodha wa timu ya Taifa Charles Venance 4-2.Dar es Salam mwishoni mwa wiki.
Mchezaji wa timu ya Klabu ya Mpo Afrika na Nahodha wa timu ya Taifa, Charles Venance akicheza wakati wa mechi ya fainali dhidi ya klabu ya Sun City wakati wa mashindano ya Safari Pool Taifa Ngazi ya Mkoa,Mkoa wa Temeke iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU