Mario Balotelli amefungiwa Mechi 3 kwa
kutumia ‘vitisho na matusi’ dhidi ya Refa mara baada ya Mechi ya Serie A
Juzi ambayo Timu yake AC Milan ilichapwa Bao 2-1 na Napoli Uwanja wa
kwao San Siro.
Balotelli alitolewa kwa Kadi Nyekundu
baada ya Mechi hiyo kwisha kufuatia kupewa Kadi ya Njano ya Pili baada
ya yeye kuvaana na Mchezaji wa Napoli Valon Behrami na kisha kuanza
kukwaruzana na Refa Luca Banti.
Katika Mechi hiyo, Balotelli alikosa
Penati iliyookolewa na Kipa wa Napoli, Pepe Reina, na baadae kupiga
shuti lililogonga mwamba na Dakika za mwisho kuifungia AC Milan hilo Bao
lao moja kwa Shuti murua.
Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa kwa Balotelli kukosa Penati tangu aanze Soka la Kulipwa.
AC Milan haijasema lolote kama itakata
Rufaa kupinga Kifungo hicho na kama kitabaki kama kilivyo basi Balotelli
atazikosa Mechi za Serie A dhidi ya Bologna, Sampdoria na Juventus.
Wakati huon huo, Wasimamizi wa Soka huko
Italy wameamuru AC Milan kufunga Jukwaa lao la Uwanja wa San Siro
linaloitwa Curva Sud kwenye Mechi ijayo na Sampdoria kama Adhabu kwa
Mashabiki waliokuwa wakighani Kibaguzi wakati wa Mechi waliyofungwa na
Napoli.
0 maoni:
Post a Comment