BENDTNER KURUDI ARSENAL BAADA MIAKA MIWILI
Nicklas Bendtner anatarajiwa kuichezea
Arsenal kwa mara ya kwanza baada ya Miaka miwili wakati Arsenal
watakaposafiri kwenda kucheza na West Brom kwenye Mechi ya Raundi ya
Tatu ya Capital One Cup.
Tangu ajiunge na Arsenal Mwaka 2005, Bendtner ameshindwa kutulia na kupata Namba ya kudumu na mara 3 ametolewa nje kwa Mkopo.
Kabla Msimu huu kuanza, Bendtner alilazimika kurudi tena Arsenal baada ya kushindwa kupata Klabu ya kuhamia.
Uwezekano wa Bendtner kucheza Mechi na
West Brom ulitobolewa na Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ambae
alisema: “Jumatano tuna Mechi na WBA ya Capital One Cup na Bendtner ana
nafasi kucheza. Kubadilisha Kikosi ni muhimu kwani Jumamosi tunacheza na
kisha inakuja Mechi muhimu mno na Napoli ya UFA CHAMPIONZ LIGI.”
Mara ya mwisho Bendtner kuichezea
Arsenal ni Agosti 2011 walipofungwa 2-0 na Liverpool na baada ya hapo
alipelekwa kwa Mkopo huko Sunderland na Juventus.
Lakini mara baada ya kuchukuliwa kwa
mkopo wa Msimu mzima na Sunderland hapo Mwaka 2011, Bendtner alitamka:
“Sitarudi tena Arsenal. Ikiwa ni juu yangu, sitacheza nao tena!”
RVP KURUDI NA LIVERPOOL!!
David Moyes amethibitisha kuwa Robin van
Persie hakuumia sana kiasi cha kumfanya aikose pia Mechi ya Manchester
United ya Jumatano na Liverpool Uwanjani Old Trafford ambayo ni ya
Raundi yA Tatu ya Capital One Cup.
Jumapili, Van Persie hakucheza kwenye Mechi ya Ligi Kuu England huko Etihad walipofungwa 4-1 na Man City.
Moyes alisema: “Tunafikiri yuko sawa. Tutampa kila nafasi. Hakuumia sana.”
Moyes alibainisha kuwa Staa huyo alikuwa
akisikia maumivu kidogo kwenye Nyonga na ili kumlinda asijiumize zaidi
waliamua kumpumzisha kwenye Mechi na Man City.
Lakini, baada ya Jumapili kufungwa na
Mahasimu wao Man City, Mechi hii na Mahasimu wao wakubwa zaidi na wa
Kihistoria, Liverpool, sasa imekuwa ya kusaka ushindi wa kufa na kupona
na upo umuhimu kwa Man United kubahatisha kwa kumuanzisha Mfungaji wao
Bora kabisa.
0 maoni:
Post a Comment