Mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi akiongea wakati wa halfa ya
kuwapongeza timu akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa
timu ya Airtel Rising stars mara baada ya kufanya vizuri katika
mashindano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria. halfa hiyo ilifanyika
jana katika hoteli ya Hyatt
katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah
akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel
Rising stars mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel
Rising Stars nchini Nigeria. halfa hiyo ilifanyika jana katika hoteli ya
Hyatt
Kocha wa timu ya wasichana ya Airtel Rising stars Rogatician Kaijage
akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel
Rising stars mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel
Rising Stars nchini Nigeria. halfa hiyo ilifanyika jana katika hoteli
ya Hyatt
Wachezaji waliozawadia kwa kungara katika michuano ya Airtel Rising
stars pamoja na captain wa timu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni
rasmi Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo (mwisho
kushoto) katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile
Osiah.
Naodha wa timu ya wasicha ya Airtel Rising Stars chini ya umri wa miaka
17 Stumai Abdalah akimkabidhi kombe la ubingwa Mkurugenzi wa maendeleo
ya michezo nchini Leonard Thadeo baada yakuwa mabingwa katika mashindano
yaliofanyika nchini Nigeria jumapili. Kushoto ni mkurugenzi wa masoko
wa Airtel Levi Nyakundi na katikati ni katibu mkuu wa shirikisho la
mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.
Kaptain ya timu ya wasichana Stumai ……. Akikabithi cheti cha kushinda
kwa Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo baada
yakuwa mabingwa katika mashindano yaliofanyika nchini Nigeria jumapili.
Kushoto ni mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi na katikati ni
katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.
Mchezaji wa timu ya wasichana Neema Paul pamoja na Mkurugenzi wa
maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo wakionyesha mfano wa hundi ya
dolla 10,000 iliyokabithiwa kwa timu ya washichana na Airtel baada ya
kuibuka washindi wa michuano ya Airtel Rising stars Afrika Kushoto ni
mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi na katikati ni katibu mkuu
wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.
Wachezaji wa timu ya wavulana wakiwa katika picha ya pamoja mara baada
ya halfa ya kuwapongeza iliyofanyika katika hotelya Hyatti jijini Dar es
salaam, pichani kutoka kushoto Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo
nchini Leonard Thadeo, wakurugenzi wa Airtel , mkuu wa shirikisho la
mpira wa miguu nchini Angetile Osiah pamaoja na Salim Madadi wa TFF
Yashauri sekta binafsi kusaidi katika michezo.
Mkurugenzi
wa maendeleo wa michezo nchini bw Leonard Thadeo ameipongeza timu ya
wasichana ya Tanzania baada ya kutwaa ubingwa wa vijana chini ya umri wa
miaka 17 ya Airtel Rising Stars yaliomalizika juzi nchini Nigeria.
Tanzania
waliibuka mabingwa baada ya kuwafunga Kenya katika fainali, pia
amewapongeza wavulana baada ya kufikia hatua ya nusu fainali. Mabingwa
wamezawadiwa kombe pamoja na kitita cha dola za marekani 10,000.
Katika
pongezi zake pia amewapongeza wafungaji kwa upande wa wasichna ni
Shelda Boniface na mvulana ni Athanas Mdamu na pia amempongeza
mchezaji bora kutoka timu ya wasichana ambae ni Tatu Iddi .
Katika
mashindano haya Tanzania imetoa rekodi tatu , mfungaji bora kwa upande
wa wasichana magoli matano, mfungaji bora wa kiume magoli manne ,
mchezaji bora kwa upande wa wasichana na pia wachezaji watatu upande wa
wavulana wamefunga magoli matatu katika mechi moja (hat-trik) na
kuondoka na mpira kila mmoja.
Kabla
ya kukabidhiwa kombe na mabingwa hao , Mkurugenzi wa maendeleo ya
michezo nchini bw Leonard Thadeo amesema kuwa serikali kupitia wizara ya
michezo itaendelea kusaidi mpira wa vijana wenye umri mdogo ili
kuifikisha mbali Tanzania katika medani ya soka.
Akiongea
kwa niaba ya msafara wa timu kocha Rogacian Kaijage amesema kua
mashindano yalikua magumu ila wamefanikiwa kuchukua ubingwa ,
amewapongeza vijana wake , kocha mwenzie wa timu ya wavulana Abel Mtweve
na pia ameishukuru Serikali , Airtel , TFF, pamoja na DRFA
Mkurugenzi
wa masoko wa Airtel bw Levi Nyakundi ameahidi kuwa Airtel itaendelea
kudhamini mpira hasa wenye umri mdogo na pia kuongeza mikoa ya ushiriki
wa mashindano ya Airtel Rising Stars .
0 maoni:
Post a Comment