Saturday, October 26, 2013

TANZANITE YAIBUKA NA KAPU LA MAGOLI

Timu ya taifa ya soka ya wanawake U20 ya Tanzania imeshinda kwa mabao 10-0 katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2013.

Timu hiyo maarufu kama Tanzanite, imefanikiwa kushinda kwa mabao hayo leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Tanzanite ndiyo walikuwa kiboko katika mchezo huo huku wakiwapa wakati mgumu wageni wao.

Kama wangekuwa makini, Tanzanite wangeweza kufuzu hata mabao zaidi ya 15 kwa kuwa walimiliki mchezo wote.

Mashabiki wa Msumbiji walionekana kuwa na jazba na kuporomosja lawama kwa benchi lao la ufundi kwamba timu yao ilikuwa nyanya.
 
Wakati huo, kinadada wa Msumbiji walionekana wakilia kwa uchungu ikiwa ni kuonyesha kutokukubaliana na kipigo hicho.
 
Kikosi cha Tanzanite
Kikosi cha Mozambiq

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU