Mrembo wa Taifa Redds Miss Tanzania 2013 Happiness
Watimanywa yuko Kampala Uganda kwa mwaliko rasmi kutoka kampuni ya Arapapa
Fashion House & Design ya nchini Uganda.
Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa
atakuwepo nchini Uganda kwa muda wa siku 5 hadi tarehe 9 Novemba 2013
anatarajiwa kurejea nchini.
Akiwa nchini Uganda ataungana na warembo wengine
kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Kenya, Rwanda, Burundi na
wenyeji Uganda.
Pamoja na mambo mengine warembo hao watahusika pia
katika kazi za jamii na baadaye kupanda jukwaani pamoja katika onyesho la
mavazi lililoandaliwa na Kampuni hiyo.
Kampuni ya Arapapa imekuwa ikifuatilia kwa karibu
mashindano ya urembo ya Miss Tanzania tangu mrembo Happiness anyakue taji na waliazimia kumualika mrembo
huyo kutembelea Uganda, jambo ambalo wamelitimiza.
Redds Miss Tanzania 2013 ambaye ni mwanafunzi wa mwaka
wa kwanza wa Shahada ya Juu katika Chuo
cha Strathclyde nchini Scotland, ameamua
kuahirisha masomo yake kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi hapo atakapovua taji
mwishoni mwa mwaka 2014.
Mrembo Happiness Watimanywa atawakilisha Tanzania
katika mashindano ya urembo ya dunia hapo mwakani.
0 maoni:
Post a Comment