Sunday, January 5, 2014

MWILI WA MAREHEMU WILLIAM MGIMWA UMEAGWA KWENDA IRINGA KWA MAZISHI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakiifariji familia ya marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga na kutoa heshima za mwisho zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilala, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko
 Mawaziri wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Dkt. William Mgimwa wakati likipakiwa kwenye gari tayari kuanza safari ya kuelekea Uwanja wa ndege kuelekea mkoani Iringa kwa maziko
                                              Mama Maria Nyerere, akitoa heshima za mwisho
                                   Spika wa Bunge Anne Makinda, akitoa heshima za mwisho.

                          Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana heshima za mwisho
                               Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, heshima za mwisho.

               Baadhi ya Mawaziriki wakiwa katika foleni kuelekea kutoa heshima zao za mwiho.

                                                          Mwili ukipakiwa kwenye gari
                                  Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakiwa katika shughuli hiyo.

                                              Baadhi ya viongozi wa Serikali waliohudhuria shughuli hiyo.

                                                    Baadhi ya Wabunge waliohudhuria shughuli hiyo

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU