Wednesday, January 8, 2014

YANGA HIYO UTURUKI

Timu ya Yanga inatarajiwa kuondoka leo usiku kwa ajili ya kambi ya siku 14 nchini Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara na Klabu Bingwa Afrika.

Kikosi kizima cha Yanga chini ya Kocha Boniface Mkwasa, kinaondoka leo baada ya kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Bora jijini Dar.

Kambi hiyo itakuwa jijini Antalya ambako Yanga iliwahi kuweka kambi chini ya Kocha Ernie Brandts aliyetimuliwa.

Msemaji wa yanga baraka amesema kila kitu kipo tayari kwa safari wanahitaji kukaa nje kwa muda wa wiki mbili ili kukinoa kikosi chao waweze kujiandaa na mzunguko wa pili na michuano ya kimataifa.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU