Monday, January 24, 2011

KILI MUSIC AWARD MACHI 26 MWAK A HUU

Tuzo za muziki   mwaka 2011,maarufu kama KILI MUSIC AWARDS zitafanyika MACHI 26 mwaka huu  zikiwa zimefanyiwa maboresho ili kuondoa malalamiko kwa wasanii.

Akitangaza mbele ya waandishi wa habari meneja wa bia ya KILIMANJARO ambao ndio wadhamini wa tuzo hizo ,GEORGE KAVISHE amesema kuwa mwaka huu kutakuwa na mabadiliko makubwa  na wataboresha mambo mbali mbali.

KAVISHE amesema kuwa kati ya mambo yaliyoboreshwa ni pamoja na wataalamu wa kuchagua wasaniii hao  na kazi zao pamoja na majaji ambapo wana uhakika wataifanya kazi hiyo kwa haki na ubora unaotakiwa.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka BASATA ANGELO LUHALA amesema kuwa watahakikisha tuzo za mwaka huu zina ubora wa aina yake na kuondoa malalamiko katika jamii.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU