Monday, January 24, 2011

KOZI YA FIFA YAANZA JIJINI DSM

                Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo NCHIMBI akikabidhiwa nembo ya FIFA
                                  Washiriki wa kozi ya FIFA
                               Ndani ya ukumbi wa kozi ya FIFA.

Waziri wa Vijana,Habari utamaduni na Michezo  NCHIMBI amewataka viongozi wa soka nchini kuitumia vyema elimu inayotolewa na shirikisho soka duniani FIFA  ya uandaaji wa matukio ya michezo ili kuondokana na miogogoro mbali mbali ambayo  hujitokeza.

Ameyasema hayo wakati wa semina maalumu  ya uandaaaji wa matukio na FIFA kwa ushirikiano na TFF ambayo inawajumuisha watendaji mbali mbali katika vilabu vya soka ,wadhamini na mameneja wa viwanja vya soka   nchini ambapo amesema wakiutumia vyema wataweza kuboresha katika mambo mbali mbali na hatimaye mambo yataendeshwa katika hali nzuri.

Wakufunzi wa mafunzo hayo wametoka katika idara mbali mbali za shirikihso la soka FIFA, wakiwemo watu  wa masoko, ambapo semina hiyo ifanyika kwa wiki moja.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU