Saturday, January 22, 2011

MANJI ASEMA YUPO TAYARI KUTOKA IWAPO MKUTANO MKUU WA YANGA UTAAMUA ATOKE

                                               MANJI akiwa ofisini kwake akizungumza na waandishi
Wakati NCHUNGA akigoma kung’oka klabuni hapo mdhamini wa klabu hiyo ya JANGWANI YUSUPH MANJI amesema yupo tayari kuondoka endapo wanachama wa klabu hiyo watataka aondoke huku akitaka wanachama hao waitishe mkutano utakowezesha kukutanisha pande zote zinazotofautiana.

MANJI amesema haya yote yanatokea kutokana na barua yake aliyoandika tarehe 12 DECEMBER mwaka jana kwa kila mtendaji wa baraza la utendaji la YANGA na viongozi hao wa YANGA walikaa na MANJI na kuamua mambo mengi ikiwa ni pamoja na MILIONI 100 ya usajili wa dirisha dogo.

Vilevile katika kikao hicho viongozi hao wa pamoja na mdhamini wao walikubaliana kuwa waongeze baraza la udhamini ili wadhamini wa klabu hiyo ya jangwani wafikie watu watano na hivyo MANJI alipendekeza mbunge mmoja wa DSM kwa kuwa klabu ya YANGA ni ya DSM.

MANJI pia ametoa sababu za kupendekeza mbunge wa DSM kuwa ni kuisadia klabu hiyo katika kupata hati ya JANGWANI kutoka wizara ya ardhi, kusaidia mawasiliano wizara ya michezo kwa ajili ya uwanja wa taifa na pia kusaidia mawasiliano wizara ya fedha kwa ajili ya kodi inayokatwa klabu hiyo.

MANJI anasema hayo yote yalikubalika katika kikao hicho ambacho kinadaiwa kuwa ni batili.

Aidha MANJI amesema kama YANGA inaona jina la mbunge alilopendekeza kuwa si zuri basi wapendekeze jina lingine

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU